Kivu ya kusini/ Kalehe: Shirika nyipya la raia lalaumu hali ya usalama mdogo wilayani humo

Shirika nyipya la raia wilayani Kalehe lalaumu hali ya usalama mdogo inayotanda eneo la milima mirefu. Hali inayo sababishwa na kundi zenyi kumiliki silaha.

Kutokana na Prezidenti wa shirika hilo nyipya la raia wilayani Kaleh Didier Misuka , kundi hilo lina sababisha usalama mdogo na hata unyanyasi.

Hawa wakilazimisha kila raia kulipa pesa 1000 franka za Kongo ambazo wanaita  » lala Salama ». Wakinena kwamba pesa hizo zawasaidia kwa mahitaji mbali mbali. Na yote yanatendeka machoni mwa viongozi wa serkali, ambao hawafanye lolote lile..

Didier Misuka ashukuru juhudi za jeshi la taifa FARDC, akiwaomba kuongeza juhudi, ili kukomesha kundi hilo lenyi kukwamisha maendeleo kwenyi milima mirefu ya Kalehe.

Chumba cha wandishi.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire