Kivu ya kaskazini : Operesheni ya orotha ya wachaguzi imeanza rasmi hii alhamisi

Ni hii alhamisi tarehe 16 februari 2023 ndiyo orotha ya wachaguzi ilianzishwa Jimboni Kivu ya kaskazini. Kazi zilianzishwa rasmi mjini Goma akiweko liwali mwanajeshi wa jimbo la Kivu ya kaskazini Constant Ndima Kogba, viongozi wa tume huru ya uchaguzi CENI na wengine wengi wa jimbo. Umati wa watu ulionekana asubui mapema kwenyi shule Nazaréen mjini Goma ambako kazi zilianzishwa.

Mnenaji makamu wa tume huru ya uchaguzi CENI nchini DRC Paul Muhindo alialika raia kuja kwenyi senta za uchaguzi ili kutimiza shurti za uraia.

« Tumeanzisha Operesheni ya orotha ya wachaguzi kwenyi jimbo la Kivu ya kaskazini pasipo wilaya za Masisi, Rutshuru na eneo moja la Nyiragpngo, nafasi zinazovamiwa na waasi wa M23. Serkali atakapo weka usalama maeneo hayo ndipo tutakwenda kuorodhesha raia.  » Anena Paul Muhindo mnenaji makamu wa tume huru ya uchaguzi nchini DRC.

Akiongeza kwamba wahami ambao walikimbilia kwenyi miji kadhaa za wilaya za jimbo la kivu ya kaskazini yaani Beni, Butembo na kadhalika wataorodheshwa nafasi waliko.

Paul Muhindo asisitiza akiomba mara tena raia kujielekeza wengi kwenyi nafasi za uchaguzi, ili wapate kadi nyipya. Kwa kuwa zile za zamani zimepigwa marufuku . Kwa kungojea kadi za uraia baadae, sherti kila mkongomani ajiorodheshe. Kiongozi huyo wa Tume huru ya uchaguzi alitowa tahazari kwa mtu yeyote asiye mkongomani akijaribu kujiorodhesha. Anaponaswa atatupwa korokoroni. Pia kwa yeyote atakae omba pesa ili kuorodhesha mtu ataazibiwa vikali.

Tufahamishe kwamba hii ni eneo la tatu la uchaguzi ambalo linajumwisha majimbo saba yaani, Bas Uélé, Haut Uélé, Ituri, Kivu ya kaskazini na ya kusini na Tshopo na Maniema. Vifaa vya kazi vinapelekwa kwenyi eneo kadhaa jimboni Kivu ya kaskazini.

Juvénal Murhula.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire