Goma: Jean Luc Mutokambali aomba raia kuwa na tumaini kuhusu maisha bora ya kesho

Katika mazungumzo na wandishi habari, akitokea mjini Kinshasa, Prezidenti wa chama cha kisiasa ULDU Jean Luc Mutokambali anena kuja likizoni ili kukutana na wachaguzi wake, wanao sumbuka miaka chungu télé. Akiwaomba kutokata kitumaini kuhusu maisha ya kesho

Gisi munavyofahamu, jimbo hili lina matatizo mengi. Nakuja likizoni kukutana na wachaguzi wangu, ambao naomba wakuwe na matumaini. Inchi yetu imekumbwa na shida tangu awali. Tuna matumaini kwa kuwa askari jeshi wetu wanaendelea kufanya kazi..

Akihojiwa kuhusu harakati za uchaguzi nchini, Prezidenti wa chama cha kisiasa ULDU anena kuunga mkono kazi hiyo, ili kuchagua viongozi wanaofaa.

Jean Luc Mutokambali asema pia kwamba chama chake cha kisiasa ULDU kinachapa kazi zake vilivyo,<< Sisi ni chama kinacho simama imara. Hatuko chama chenyi kupiga tu kilele tu kama vyama vimoja vingine. Tunafanya kazi bila shaka>>, aeleza mzaliwa huyu wa wilaya ya Rutshuru.

Juvénal Murhula.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire