Goma: Serge Lukwebo aomba raia wawe na umoja wakati huu wa shida zinazo wakumba

Akiwasili mjini Goma toka mji mkuu Kinshasa, Serge Lukwebo mtoto wa Prezidenti wa chama cha kisiasa AFDC Bahati Lukwebo aalika raia wa DRC, hususan wa jimbo la Kivu ya kaskazini kwa umoja katika hali hii ya vita.

<<Tunataka umoja wakati huu wa shida. Jimbo letu linapitia hali ngumu kutokana na usalama mdogo. Tunaomba raia wawe makini, na wajihusishe ndani harakati hizo. Inabidi kuchukuwa hatua ili kujuwa aina gani ya viongozi raia wanahitaji. Raia wajihushe na harakati za uchaguzi kupitia hali tunayoishi kwa sasa. Kwetu ni fursa ya kuomba wawe na umoja na mazungumzo>>, anena Serge Lukwebo.

Tufahamishe kwamba Serge Lukwebo alikuwa akijibu kwa maswali ya wandishi habari kwenyi uwanja wa ndege mjini Goma, jimboni Kivu ya kaskazini.

Juvénal Murhula.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire