Kivu ya kaskazini : Norbert Basengezi Katintima atowa pole kwa wahanga wa vita vya M23

Akiwa ziarani mjini Goma tangu hii alhamisi tarehe 2 machi 2023 Mwenyekiti wa chama cha kisiasa ANCE Norbert Basengezi Katintima atowa mkono wa rambi rambi , kwa jamaa zote zinaendelewa kukumbwa na misiba. Ikisababishwa na vita vya M23 wakiwa upande wa nchi ya Rwanda jirani. Huyu akipokelewa na umati kwenyi uwanja wa ndege.

Alipofika kwenyi makao yake ndani ya mji wa Goma, Norbert Basengezi Katintima alionyesha ujumbe mkubwa toka pembe zote za Jamhuri ya kidemokrasia ya kongo, wakimsindikiza katika ziara yake.

Mwenyekiti wa chama Alliance des Nationalistes pour un Congo Nouveau kwa kimombo, aliomba pia raia jimboni kuweza kujiorodhesha ili waweze kushiriki kwenyi harakati za uchaguzi nchini mwao. Akiongeza kwamba chama cha kisiasa ANCE kinamuunga mkono Raisi Félix Antoine Tshisekedi Tshilombo.

Aliendelea kulaumu shambulizi la DRC na nchi ya Rwanda, hali inayokwamisha usalama mashariki mwa nchi hiyo.

Pamoja na hayo Norbert Basengezi Katintima aliyekuwa Prezidenti makamu wa tume huru ya uchaguzi CENI nchini DRC, alisema kwamba atatembelea wahami wa vita vya M23 kwenyi kempi ya Kanyaruchinya. Hiyo ni moja wapo mwa kazi nyingi alizozifanya kwa manufaa ya wakongomani nchini kote. Akinena kuwaletea wahami blanketi, bâches, maji na kadhalika.

Juvénal Murhula.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire