Kutokana na mwenendo mubaya katika orodha ya wachaguzi mashariki mwa DRC hususan jimboni Kivu ya kaskazini, Mwanabunge wa taifa Jean Baptiste Kasekwa aomba iongezwe muda ya orotha ya wachaguzi hadi tarehe 14 juni jimboni Kivu ya kaskazini. Akilaumu nia mbaya yake Prezidenti wa tume huru ya uchaguzi Denis Kadima katika maandalizi ya orotha ya wachaguzi.
Mwanabunge wa taifa Jean Baptiste Kasekwa alinena hayo wakati wa kongamano ya mazungumzo alioandaa mjini Goma hii ijumaa tarehe 25 machi 2023.
Jean Baptiste Kasekwa akisisitiza kuhusu wilaya za Masisi, Rutshuru na Beni ambazo ni wahanga wa vita vya waasi wa M23 na wale wa ADF. Akiangazia kwamba ingawa maeneo hayo hayata orothesha wachaguzi wengi, jimbo la Kivu ya kaskazini litapoteza viti vingi bungeni
Mwanabunge wa taifa Jean Baptiste Kasekwa aligusia pia kutoendelea vema kwa orotha ya wachaguzi kwa kuwa tume huru ya uchaguzi CENI hailipe wafanya kazi pesa zao. Pamoja na hayo hali mbaya ya kompyuta ambazo zinatowa pia hali mbaya ya kadi ya wachaguzi. Kwa hiyo Mwanabunge wa taifa Jean Baptiste Kasekwa aomba wafanya kazi wa tume huru ya uchaguzi kuanza mgomo hadi watakapo lipwa pesa zao.
Mwanabunge huyu akizania kupokonya nusu ya pesa kiwango cha dola milioni 30 ziilizoandaliwa katika harakati za orotha ya wachaguzi. Kwa kuwa uchaguzi uliopita tume huru ya wachaguzi ilitumia milioni 64 dola za marekani na kutowa kazi iliyo halali. Jean Baptiste Kasekwa kujiswali kwa nini wakati huu Tume huru ya uchaguzi CENI hutumia milioni 94 dola za marekani bila kuonyesha kazi iliyo halali. Mfano wa kompyuta zenyi kuharibika kila wakati zikitowa kadi zinazoweza haribika kwa haraka.
Mwanabunge huyu wa taifa anaomba raia kuendelea kuwa makini ili uchaguzi ufanyike tarehe 20 disemba 2023. Kama sivyo kulazimisha kipindi cha mseto ambacho wakongomani wataamuwa kuhusu yule atakaekiongoza hadi uchaguzi iandaliwe.
Juvénal Murhula.
Poster un Commentaire
Vous devez vous connecter pour publier un commentaire.