Goma : Akina mama wafurahiswa na kufunguliwa kwa akaunti 1000 naye Bi Juliette Mbambu Mughole kwenyi CADECO

Kiongozi husika na benki ya taifa CADECO Bi Juliette Mbambu Mughole ameshukuru kwa kumlaki raia mjini Goma, miongoni akina mama wengi, ambao wamekubali maoni yake Raisi wa taifa Félix Antoine Tshisekedi, inayo lenga kukomesha umaskini nchini DRC. Na hiyo kupitia benki ya taifa CADECO.

<<CADECO ni benki moja nchini kwa manufaa ya raia. Maoni yake Raisi wa taifa ni kupiganisha umaskini. Ilibidi nije kuhamasiha ndani ya miji ambamo benki CADECO lapatikana. Nikifunguwa akaunti 1000 kuhusu waanzilishi wa kazi na hata akina mama wenyi kufanya kazi ndogo ndogo. Tumetambuwa mapokezi makubwa. Ni kwamba raia wamesikia maoni yake Raisi wa taifa kwenyi eneo hizi za vita. Ijapo Raisi aendelea kupiganisha hali ya vita eneo hizi za vita, anatamani pia kutowa mchango kidogo, ili kuinuwa hali ya uchumi ndogo,>> aeleza kiongozi wa benki CADECO Bi Juliette Mbambu Mughole mbele ya wandishi habari.

Huyu alinena kufurahishwa na mazungumzo naye liwali mwanajeshi Constant Ndima Kogba ambaye aliahidi kuunga mkono maoni yake Raisi wa taifa. Bi Mbambu Mughole ambaye pia ni Prezidenti wa chama cha kisiasa ACLP alikubali kuunga mkono maoni yake Raisi. Akisisitiza kwamba inabidi kufanya kazi kwa kungojea mwisho wa vita.

Prezidenti wa chama cha kisiasa ACLP anena kufurahishwa na masemi yake liwali wa jimbo la Kivu ya kaskazini.

<<Aliahidi kuunga mkono maoni yake Raisi wa taifa Félix Antoine Tshisekedi. Na kutusindikiza katika kazi hii ambayo si rahisi kulingana na hali ya vita jimboni. Liwali aliomba kufika kaskazini mwa Kivu ya kaskazini eneo kubwa la vita. Na hata kuwatembelea wahami wa vita eneo kadhaa za jimbo, ili wapewe nayo mikopo midogo midogo kwa kungojea,>> Bi Juliette Mbambu Mughole aongeza.

Upande mwengine, kiongozi wa benki CADECO jimboni Kivu ya kaskazini ashukuru akina mama, kwa kujibu wengi kwa aliko la benki CADECO.

<<Kwa heshima yenu wa mama, tunasema aksanti kwa kujibu kwa sherehe hii, ambayo iliandaliwa na CADECO benki yetu. CADECO inawapenda sana. Mradi wa akaunti 1000 uliundwa ajili yenu akina mama. Tunawaomba kuinzingatia ili kuunga mkono maoni yake Raisi wa taifa. Maoni yenyi kuungwa mkono pia naye mama kiongozi wetu wa benki CADECO nchini, ambaye tunasindikiza. Mikopo mutapata. Kwa sasa tutaunda kamisheni ili kuchunguza namna akina mama wanatumika. Tutatumika pamoja na mama viongozi tunao fahamu vizuri. Tunapo chunguza kazi, ndipo tutajifunza la kufanya, na baadae kupana kitu kidogo,>>afasiria kiongozi. Kiongozi wa CADECO

Huyu aongeza kwamba vikao aina hiyo vitaendelea, ili kupiganisha umaskini ndani ya jamii.

Juvénal Murhula.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire