Bwana Nzanzu Kavungira Blaise alikutana hii ijumaa tarehe 7 aprili na raia wengi wanao unga mkono Fondation hiyo ya kwake. Katika lengo la kuchunguza pamoja gisi kazi ziliweza fanyika wakati wa kufunguliwa rasmi kwa Shirika hilo kwa jina la Nzanzu Kavungira Blaise. Ilikuwa juma mosi iliyopita.
Mwanzilishi wa Fondation Nzanzu Kavungira Blaise ambayo inaitwa kwa jina lake mwenyewe alipendelea kuwa kumbusha lengo la shirika lake.
<<Hii mkutano ni kutokana na kufunguliwa rasmi kwa Shirika letu juma mosi iliyopita. Wamama, wa baba, wadada na wa kaka wakiwa wengi siku île. Tulifasiria kusema kwamba sisi ni shirika lenyi kusaidia walio wengi, kuhusu shida kijamii. Na watu walifika wengi kutusindikiza. Léo ni muda wa kufanya uchambuzi na raia waliotusindikiza. Tuliambia wa Baba, wa mama, wa dada, na hata wa kaka kama shirika Nzanzu Kavungira Blaise ni karibu kwa kuwasaidia, kuwasindikiza katika shida zao. Tuko pembeni yao na milango yetu ni wazi>>, afasiria Nzanzu Kavungira Blaise Mwenyekiti wa shirika. Akiongeza :
Sisi hatukuja kupana pesa, ila kuwasindikiza katika miradi kadhaa, kuwapa elimu, kuwaletea ujuzi, kupitia watalaam katika miradi mfano mafunzo katika kuunda kazi, kushona vitu, ufugo na kadhalika, aangazia Nzanzu Kavungira.
Raia upande wao, walisema kushukuru na kuunga mkono shirika hilo ili lisonge mbele kupitia Mwenyeji.
<<Tunashukuru Nzanzu Kavungira Blaise kwa kuunda kikundi hiki, kwa kuwa itatusaidia katika mambo mengi. Ameanzisha shirika ajili yetu wasio jiweza. Atatuhimiza kwa kazi mbali mbali za mikono. Tunaamini kwamba yote yatatekelezwa. Tuko nyima yake sana katika yote. Tunaomba wengine wakuje wengi tujenge shirika letu Nzanzu Kavungira Blaise, ambayo tayari imefunguliwa rasmi. Tutamusindikiza pia kwa mawazo yake mazuri, na tunaamini atafaulu. Wengi tulisindikiza ila haukufaulu,>>waeleza raia wengi walikusanyika kwenyi complexe ITALA.
Kuhusu mwenendo ya orotha ya uchaguzi, Nzanzu Kavungira Blaise alilaumu hali ya rushwa ndani ya senta kadhaa za orotha ya wachaguzi. <<Matatizo ni cungu tele kwenyi senta yaani hesabu ndogo ya computer, kukosa ujuzi kwa wafanya kazi kadhaa wa Tume huru ya uchaguzi na kadhalika>>, anena Mwanzilishi wa Shirika Nzanzu Kavungira. Akiomba raia kutulia, na Tume huru ya uchaguzi kutafuta suluhu kwa shida hizo.
Juvénal Murhula.
Poster un Commentaire
Vous devez vous connecter pour publier un commentaire.