Goma: Wachuuzi wa soko ya Nyabushongo waomba askari polisi wabadilishwe kwenyi soko

Wachuuzi wa soko ya Nyabushongo pa Ndosho waomba wabadilishwe askari polisi eneo hilo, kwa kuwa hawafaulu kuwalindia usalama ndani ya soko. Wananena kuwa wahanga kila mara ya vitendo vya wizi na watu wasiojulikana. Ni mara ya munane sasa wizi huwo unaonekana ndani ya soko hiyo, ijapo kuwepo kwa askari polisi.

Wachuuzi wakitowa malalamiko mbele ya wandishi habari mjini Goma hii alhamisi tarehe 6 aprili 2023.

Duru hizo zanena kwamba vitendo hivyo vyafanyika usiku, ijapo kuwepo kwa askari polisi usiku ndani ya soko. Wakijiswali kwa nini walinzi wa usalama hawaja gunduwa wanaotenda vitendo hivyo haramu kwenyi soko ya Ndosho. Wakisii viongozi wabadilishe hawa askari polisi wasiofaa kwao.

<<Ni zaidi ya mara munane wevi wanaiba ndani ya dépôt yangu. Ijapo tunakuwa na askari polisi ndani ya soko. Hatufahamu kazi ya hawa watu. Tunaomba viongozi kuwabadilisha haraka iwezekanayo. Ujumbe ya wachuuzi ilikwenda kumuona Prezidenti wa kamati ya wachuuzi, wakimupa ripoti. Askari polisi wamoja hunena kwamba kazi yao sio ulinzi wa soko. Hatuone mafaa, sherti wabadilishwe,>>aeleza akina mama moja mhanga akitowa machozi.

Prezidenti wa kamati ya wachuuzi wa soko ya Nyabushongo anena kukerwa na jambo hilo la wizi, ambalo ni kila kwenyi soko.

<<Ninasikitika na hali ambayo inaendelea kukumba wachuuzi. Kila mara natowa ripoti kwa viongozi kuhusu wizi ndani ya soko, ila hakuna suluhu. Jambo la kushangaza ni kwamba askari polisi hawa wanahudumiwa na wachuuzi kwa chakula na hata kwa pesa mara moja kwa jumaa. Ila ni wachuuzi hawa ndiyo wahanga wa vitendo vya wizi kila leo. Inabidi mimi na kamanda wao kujihusisha ili askari polisi hawa wabadilishwe. Shida ya wachuuzi wangu ni yangu pia, siwezi nikapate amani>>, aeleza kwa huzuni Bwana Makelele kiongozi wa kamati ya Nyabushongo.

Juvénal Murhula.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire