Kivu ya kaskazini : Fondation Lubungo Matayo Jules ni lenyi kuunga mkono Raisi wa taifa kuhusu maendeleo

Akizungumza na wandishi habari mjini Goma, mwanzilishi wa Fondation Lubungo Matayo Jules ambayo inaitwa kwa jina lake aomba wakongomani kwa jumla, hususan raia jimboni Kivu ya kaskazini kufanya kazi kwa bidii na kujitegemea.

Alionyesha kwamba ni katika lengo hilo, pia kujibu kwa maoni ya mashujaa ayati Mzee Laurent Désiré Kabila na Patrice Emery Lumumba, na hata ya Raisi wa taifa. Hawa wakiomba kuwa makini, kufanya kazi kwa Kujitegemea.

Mwenyeji shirika Lubungo Matayo alitaja kazi nyingi alizozifanya kwa kuchangia kwa maendeleo ya nchi bila malipo. Kukarabati zaidi ya barabara kumi pa Nyiragongo, kutowa bata za ufugo kwa wajane, kuwapa walimaji mbegu.

<<Tuhimize watu Kujitegemea. Tusiwe watu wenyi kutusi Raisi wa taifa bila sababu. Ukiwa hata msomi, usichague kazi. Fanya hata kazi za mikono. Sisi sote si mabunge, ama mawaziri. Tuunde kazi kwa kusaidia raia, tukiunga mkono Raisi wa taifa, >> afasiria Lubungo Matayo.

Akiwa pia Prezidenti wa kamati ya soko Mama Olive Lembe aliahidi kwamba shirika lake litafikia lengo hata maadui wainuke.

<<Tuko na mradi ya kufunza wajane kazi za kusuka vikapo na kushona mavazi, Mwaka huu wa shule, tuligawa buku kwa yatima, yote katika lengo la kuunga mkono maoni ya Raisi wa DRC, aeleza kiongozi Lubungo Matayo Jules. Pamoja na hayo kazi kuhusu akiba na mikopo ambazo ni miaka 2.5 tangu kuanza. Zikujumwisha kwa sasa watu elfu 3, na hata watumishi 7 ndani ya ofisi. Bila kusahau ufugo wa nguruwe, kupasuwa mawe, vijana kutengeneza gari, ujenzi wa jumba la ofisi na kadhalika,>>anena Jules Lubungo.

Tufahamishe kwamba watu kadhaa tayari wamepata makao kupitia shirika Lubungo Matayo Jules, hasa katika mradi wa akiba na mikopo, anena kiongozi huyo.

Juvénal Murhula.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire