Kivu ya kaskazini : Acheni Lukwebo Romain atowa pole kwa jamaa zilizokumbwa na msiba pa Kalehe

Mwenyekiti wa chama cha kisiasa AFDPC Acheni Lukwebo Romain yupo ziarani mjini Beni, ambako kutafanyika kongamano ndogo ya chama hicho. Akiwasili mjini Goma, huyu alitowa hongera kwa jamaa zilizokumbwa na msiba pa Kalehe kutokana na maji ya mvua.

<< Nakuja Goma. Mimi ni mtoto wa mjini. Nafikaka kila mara. Kwa sasa, niko nikipita na kujielekeza mjini Beni ambako tutaendesha kongamano ndogo>>, ahakikisha kiongozi huyo.

Acheni Lukwebo Romain alipata fursa ya kutowa pole kwa jamaa zilizo poteza ndugu zao kutokana na maji ya mvua pa Kalehe. Watu zaidi ya 400 kufariki dunia , na zaidi ya elfu 5 kupotea pasipo miili kuonekana.

<<Tunatowa pole kwa jamaa za Kalehe. Tunaomba serkali na watu wengine wa moyo mwema, kutowa msaada kwa jamaa hizo ambazo ni yatima na wajane,>> asisitiza presidenti ya chama cha kisiasa AFDPC.

Kuhusu harakati za uchaguzi, Acheni Lukwebo Romain anena kwamba chama chake ni tayari kupigania ushindi kwenyi Operesheni hiyo.

<<Niko tayari kwenda kwenyi uchaguzi kila mara, kwani maisha ni vita mtupu. Hatutachoka hata kidogo. Tuko tayari kwenyi uchaguzi kwa ngazi zote; seneti, bunge la jimbo, bunge la taifa na hata kwenyi tabaka za chini,>> aeleza kiongozi Acheni Lukwebo Romain. Akionyesha pia furaha ya kukutana na raia wa Beni, ambako wangojea kumpokea kwa shamra shamra.

Juvénal Murhula.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire