DRC : Chama cha kisiasa AVRP kinaandaa kongamano ya kwanza ili kujiandaa kwa uchaguzi

Kongamano ya kwanza ya chama AVRP kwa kimombo Action des Volontaires pour la Relève Patriotique inaandaliwa mjini Kisangani tangu tarehe18 juni 2023. Atashiriki pia Prezidenti wa chama hicho Muhindo Nzangi Butondo, ambaye ni waziri wa yunivasti nchini DRC.

Akihojiwa na wandishi habari kwenyi uwanja wa ndege mjini Goma, Mheshimiwa Kambale Kisuba Jacques anena kufurahishwa na kongamano inayo pelekea maandalizi ya uchaguzi mwezi disemba 2023. Na kwamba ni muda wa kubadili fikra kwa kuandaa mbinu kuhusu kugombea viti vya utawala Kivu ya kaskazini kwa peke na nchini DRC kwa jumla.

Kambale Kisuba Jacques anena pia kwamba watatowa maoni yao ndani ya kikao, katika lengo la kutaka kiboresha hali ya maisha nchini DRC. Akiongeza kwamba ni fursa ya kuzungumza kuhusu kandideti Raisi wa taifa, wanabunge wa taifa, wanabunge wa jimbo, viongozi wa tabaka za chini na Kadhalika.

Tufahamishe kwamba kongamano itaanza tarehe 18 hadi tarehe 20 juni 2023.

Juvénal Murhula.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire