DRC : Kongamano ya chama cha kisiasa AVRP yaandaliwa mjini Kisangani

Ni tangu tarehe 18 hadi 20 juni 2023, ndipo kutaendeshwa kongamano ya chama cha kisiasa AVRP Action des Volontaires pour la Relève Patriotique mjini Kisangani. Wanamemba wa chama hicho toka pembe kadhaa za DRC watashiriki kwenyi kongamano muda wa siku tatu.

Akihojiwa kuhusu lengo la kujielekeza kwenyi mkutano huo mkuu, Mheshimiwa Kakule Mate moja wa memba wa chama hicho anena kuwa mwenyi furaha kubwa , kuwa kushiriki kwenyi kikao.

Huyu akishukuru wakuu viongozi wa chama chake Muhindo Nzangi Butondo ambao wamejitahidi ili mkutano ufanyike. Katika lengo la kuandaa uchaguzi mwezi disemba 2023. Akiongeza kwamba chama cha kisiasa AVRP kinaendelea kushimikwa kote nchini DRC.

Kwa nini mji wa Kisangani kuchaguliwa nafasi ya kongamano ? Mheshimiwa Kakule Mate anena kwamba chama AVRP ni chama cha kitaifa. Na kwamba kongamano ya chama hicho yaweza fanyika ndani ya kila jimbo ya DRC.

Kakule Mate aongeza kuwa chama hicho ni chenyi kutafuta maendeleo ya nchi, inabidi kutumika kwa bidii ili kujinyakulia ushindi kwenyi uchaguzi ujao.

Juvénal Murhula.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire