Kisangani : Kunaandaliwa kikao cha chama cha kisiasa AVRP tangu tarehe 18 hadi tarehe 20 juni 2023

Kongamano ya kwanza ya chama cha kisiasa AVRP chake Muhindo Nzangi Butondo inaandaliwa mjini Kisangani jimboni Tshopo. Mheshimiwa Kiza Mahungu Edgar moja wa viongozi toka wilaya ya Nyiragongo anashiriki kwenyi kongamano muda wa siku tatu.

Katika mazungumzo na wandishi habari kwenyi uwanja wa ndege mjini Goma, Kiza Mahungu Edgar anena kwamba ni fursa ya kupanga kazi kuhusu harakati za uchaguzi mwaka tunao. Watafahamu ni nani kandideti Raisi wa taifa, wanabunge wa taifa, wanabunge wa jimbo viongozi wa tabaka za chini na Kadhalika.

Mheshimiwa Kiza Mahungu Edgar ashukuru wanamemba wengine wa chama chake AVRP, hasa wale tayari wamekwisha wasili mjini Kisangani.

<< Naomba sisi sote tusaidiane kwa mazungumzo ili tulete mabadiliko kamili nchini DRC>>, aeleza Mahungu Edgar. Huyu aomba raia wa wilaya yake kubaki kwa magoti, ili kazi watakazo zifanya zitowe matunda bora. Na kwa hiyo kwa manufaa ya raia wa DRC kwa jumla, hususan wale wa Nyiragongo.

Juvénal Murhula.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire