Kisangani : Espérance Mwasi angojea kushiriki kwenyi kongamano ya chama cha kisiasa AVRP

Bi Espérance Mwasi moja wa memba wa chama AVRP apatikana kwa sasa mjini Kisangani jimboni Tshopo. Akitarajiya kugombea kiti kwenyi ngazi za bunge, huyu atashiriki kwenyi kongamano inayoandaliwa na chama AVRP mjini Kisangani.

Tukumbushe kwamba kwenyi uwanja wa ndege mjini Goma, Bi Espérance Mwasi alinena kuwa mwenyi furaha kubwa kwa kushiriki kwenyi kikao. Na kwamba atakutana na wanamemba wengine wa chama.

Akishukuru wakuu viongozi hasa mwenyekiti Muhindo Nzangi Butondo kwa kuandaa kikao hicho. Pamoja na hayo, ashukuru wanamemba wenzake wa chama waliotangulia kwenyi nafasi ya kikao.

Akiwa na matumaini kwamba ni fursa kwao kuandaa vilivyo harakati za uchaguzi mwaka huu 2023 na mengineo. Tukumbushe kwamba kongamano hiyo itadumu muda wa siku tatu, tangu tarehe 18 hadi tarehe 20 juni 2023.

Juvénal Murhula.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire