Kisangani : Mheshimiwa Kakule Mate asubiri kushiriki kwenyi kongamano ya chama cha kisiasa AVRP

Mheshimiwa Kakule Mate aendesha ziara yake mjini Kisangani jimboni Tshopo.Akisubiri kushiriki kwenyi kongamano inayoandaliwa na viongozi wa chama chake AVRP, ambayo itaanza hii tarehe 18 juni kama ilivyo pangwa. Mwenyekiti wa chama ni Mheshimiwa Muhindo Nzangi Butondo ambaye ni waziri wa yunivasti nchini DRC.

Tukumbushe kwamba kwenyi uwanja wa ndege mjini Goma, Kakule Mate alisema kuwa mwenyi furaha kubwa, kwa kuwa miongoni mwa watakao shiriki kikao.

Akishukuru wakuu viongozi wa chama AVRP, hasa mwenyekiti Muhindo Nzangi Butondo, wote pamoja wakiandaa mkutano huo mkuu. Mtarajiwa mwanabunge Kakule Mate aonyesha kwamba ni fursa kwa wanamemba wa chama kutayarisha vema kazi za uchaguzi mwaka tunao na mengineo.

Bwana Kakule Mate afahamisha kwamba chama AVRP kinaendelea kutandaa kote nchini DRC.

Tukumbushe kwamba kongamano hiyo itadumu muda wa siku tatu, tangu tarehe 18 hadi tarehe 20 juni 2023.

Juvénal Murhula.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire