Kisangani : Chama cha kisiasa AVRP kimehitimisha kongamano yake

Chama cha kisiasa AVRP yaani Action des Volontaires pour la Relève Patriotique kimekomesha kikao iliyoandaliwa muda wa siku tatu mjini Kisangani. Mkutano uliohusu hasa maandalizi ya uchaguzi mwaka huu wa 2023. Ambao ulijimwisha umati wa watu.

Wanamemba kadhaa wa Goma tuliowa hoji toka mjini Kisangani wananena kwamba ilikuwa fursa ya kupanga kina nani watakao gombea kwenyi uchaguzi huo, sawa wanabunge wa taifa, wanabunge wa jimbo. Waligusia pia ideolojia ya chama hicho na kadhalika.

Muhindo Nzangi Butondo Prezidenti wa chama AVRP nchini DRC alinena kufurahishwa na chama avrp, ambacho ni kubwa nchini ijapo kiliweza kuanza hapa karibuni.

Hawa wanena kwamba walipokea shauri toka mwenyekiti wa chama Muhindo Nzangi Butondo. Akiwaeleza namna wapaswa kujitahidi ili kuwa washindi wakati huu wa uchaguzi.

Wanamemba toka mjini Goma walinena kufurahishwa kwa kutanana na wenzao wa chama, toka pembe zote za Jamhuri ya kidemokrasia ya kongo. Wakiwa Kambale Kisuba Jacques, Kakule Mate, Espérance Mwasi, Kiza Mahungu Edgar, Siyasembe na kadhalika. Mengi mutaya fahamishwa baada ya kukutana na ujumbe wa chama AVRP ambao unasubiriwa mjini Goma.

Media la ronde info inatakia wanamemba hawa ujio mwema mjini mwao pa Goma jimboni Kivu ya kaskazini.

Juvénal Murhula.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire