Akiwa ziarani mjini Goma tangu juma nne tarehe 2 julai 2023, Bi Nelly KAMANA Katibu husika na maisha ya kijamii na kupokonya silaha kwenyi wizara ya ulinzi, atoa mkono wa pole kwa raia wanao teswa jimboni Kivu ya kaskazini. Huyu akiwa mgombea kwenyi uchaguzi, alikuja kuweka vikartasi vyake kwenyi CENI, kama kandideti mjini Goma. Akieleza kwamba muungano wa chama chake CNC utatumika mkono mkononi, kuhusu ushindi wake Raisi wa taifa Félix Antoine Tshisekedi kwa uchaguzi mwaka huu wa 2023.
<<Kufika mjini Goma ni kwamba niweke vikartasi vyangu kwenyi tume huru ya uchaguzi CENI nikiwa mgombea. Nitazidi kusindikiza chama changu CNC yaani Congrès National Congolais kwa kimombo. Kikiunga mkono Raisi wa taifa Félix Antoine TSHISEKEDI TSHILOMBO, kwenyi uchaguzi huu mwaka 2023,>> aeleza Bi Nelly KAMANA.
Huyu atamani kushiriki kwenyi hatua zote zenyi kuchukuliwa kuhusu uongozi wa nchi, kutumikia nchi yake, na inabidi apate nafasi ili atumike jisi inavyofaa.
<<Nina ujumbe wa amani kuhusu hali waishimo raia jimboni Kivu ya kaskazini. Ninatamani kurudi kwa amani jimboni humo,>> asisitiza mwana siasa huyu.
Akihojiwa kuhusu kipi kilicho pelekea kuwa kandideti mjini Goma, Bi Nelly KAMANA arudilia mara tena. << Kama nilivyo tamka hapo mbeleni, ninatamani nipate nafasi ili nitumike vilivyo. Kwa kuwa mara kwa mara ujumbe haufikie kwenyi ngazi za juu. Sisi tutajitahidi ili kuufikisha kwa ngazi zinazo stahili,>> aongeza akina Mama huyu. Na kwamba atapigana kiasi ili kunyakuwa ushindi, kwa kuwa ndio kazi ya mwanabunge.
Tukumbushe kwamba Bi Nelly KAMANA alipokelewa kwa shamra shamra na umati kwenyi uwanja wa ndege, kabla ajielekeze ndani ya mji.
Juvénal Murhula.
Poster un Commentaire
Vous devez vous connecter pour publier un commentaire.