Nyiragongo : Mwanabunge MUTEULE MOROMORO aomba raia kumuunga mkono akigombea kiti bungeni

Naomba raia wa Nyiragongo waniunge mkono, wa baba, wa mama, wasichana na hata wavulana wote, kwani vita ni kubwa. Nazani tutanyakuwa ushindi, sisi kama muungano wa kisiasa BUREC, mwakilishi ambaye ni Julien Paluku KAHONGHYA. Nina imani. Ndio maana nasii raia waanze kutanana moja kwa moja, bila kungojea. Kupita mlango kwa mlango, ili kufasiria raia kazi kubwa tulizozitekeleza wakati wa mhula.

Hayo ni miongoni mwa lengo zilizo pelekea mwanabunge wa taifa mzaliwa wa Nyiragongo Muteule MOROMORO kufika mjini Goma, kwa kupeleka vikartasi vyake kwenyi Tume huru ya uchaguzi CENI, akigombea nafasi bungeni.

<<Mbele ya yote, tunashukuru Mwenyezi Mungu kwa yote aliyotutendea. Pamoja na hayo, tunashukuru mwenyekiti wa muungano wa kisiasa BUREC Julien Paluku KAHONGYA, ambaye aliweza jitahidi kwa kurahisisha safari. Nashukuru pia wanamemba wa shirika Musisimuke, ambao walitowa mchango ili tufaulu. Mimi sikutowa kitu chochote kwa kazi hii. Ninayo furaha kubwa moyoni mwangu. Nazani kwetu Nyiragongo ni umoja pasipo mgawanyiko,>> anena Mwanabunge MUTEULE MOROMORO.

Akiongeza kwamba kazi ni nyingi za kufanya, ila zimoja tayari zimekwisha kutekelezwa.

<<Katika sekta ya maadibisho; tuliunda mashirika kadhaa. Viongozi wa mahali wanakuwa na ofisi ambazo zilijengwa na pesa zetu binafsi. Hii ni moja wapo wa yale tutaeleza wakati wa kampeni. Kuna kazi zingine zilifanyika ndani ya sekta ya afya. Kuhusu mendeleo, tulijitahidi kwa ujenzi wa barabara na mengineo. Nazani tuko miongoni mwa wale wanaojitowa kuhusu maendeleo ya Nyiragongo, tukiwa na moyo wa kupenda raia. Ni kwao kuanza kufungua macho. Ifikapo wakati wa uchaguzi, kuweza kuchagua vilivyo,>> akitowa shauri kwa umati uliokuja kumlaki.

Baadae alizungumza na wanamemba wa shirika MUSISIMUKE kuhusu mwenendo wa kazi

Juvénal Murhula.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire