Kivu ya kaskazini : Jonas Kasimba moja wa wafanya bishara jimboni yupo miongoni mwa wagombea kwenyi bunge la taifa

Akiwasili mjini Goma hii juma tano tarehe 26 julai Jonas Kasimba akiwa mfanya bishara anena kwamba amechukuwa hatua ya kwenda bungeni, ili kutetea raia wa jimbo la Kivu ya kaskazini kwa jumla n’a wale wa Beni kwa upeke, ili kupata suluhisho kwa shida zinazo wakumba kila leo.

Alinena hayo kwenyi uwanja wa ndege mjini Goma, mbele ya wandishi habari, akitokea mjini Kinshasa.

<< Mimi ni kandideti kwenyi bunge la taifa kutoka Beni. Mbele ya yote, mimi ni mfanya bishara. Ila wahenga wanena; ingawa haujihusishe na siasa, siasa itajihusisha na wewe. Tunazani kwamba ni muda sasa wa kushiriki kwenyi uongozi wa nchi. Kwa kuwa tutashiriki kwenyi uongozi wa nchi, tunaamini kwamba tutaleta mchango wetu kwa ujenzi wake. Na ndio ilipelekea sisi kuwa kandideti,>> afasiria mfanya siasa ambaye pia ni mfanya bishara Jonas Kasimba.

Akihojiwa kuhusu kile atakacho kifanya kutokana na usalama mdogo akiwa bungeni; yeye anena kwamba ata shurtisha serkali kuleta suluhu kwa shida hiyo, ila si yeye kuleta suluhisho kama mwanabunge.

Jonas Kasimba asema kuwa na moyo wa furaha kuona raia wa Beni kumtuma kama mwanabunge wao.

<<Mimi nina moyo wa furaha. Sikuzani kwamba jambo hili litafika. Siwezi kupinga matakwa ya raia. Na ndio maana nilichukuwa hatua ya kujibu kwa mwito ule, nikiwa kandideti kwenyi bunge la taifa kutoka Beni,>> asisitiza kandideti huyu mwanabunge.

Juvénal Murhula.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire