Habari kutoka mjini Bukavu zaeleza kwamba nyumba kadhaa pamoja na shule zimewaka moto hii usiku ya juma mosi tarehe 29 julai 2023 kwenyi mashanga njia ya shule INSTIBA, mtaani Bagira. Ila hatuja fahamishwa matokeo kamili ya ajali hiyo ya moto na hata chanzo.
Tukibaki katika ukrasa huo tueleze kwamba, kampyuta mia tisa 900 zikitayarishwa kwa kazi za uchaguzi kwenyi Tume huru ya uchaguzi CENI ngambo ya shirika SNCC mjini Bukavu, zimeteketea pia kwa moto. Ajali ilifanyika usiku wa ijumaa kuamkia juma mosi tarehe 29 julai 2023 majira ya saa saba usiku.
Duru za mahali hunena kwamba ni jumba la kuweka vifaa vya Tume huru ya uchaguzi CENI ndilo liliwaka moto usiku huo, bila msaada wowote.
Tufahamishe kwamba ni siku chache kabla ya kuripotiwa ajali ingine ya moto ndani ya kata Nyamugo mtaani Kadutu. Ajali iliyo teketeza nyumba karibuni kumi, zikiwaka mto mchana kati. Vifaa vya nyumbani vilichomwa kwa moto wakati huo.
Wandishi.
Poster un Commentaire
Vous devez vous connecter pour publier un commentaire.