DRC/ UCHAGUZI : Raia hujiswali ni akina nani wachaguwe watakao watumikia vilivyo

Raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo waendelea kujiswali ni akina nani wakandideti waweze kuchaguwa, kwa kuweza kuwatetea, ili kukomesha hali mbovu ambamo waishi kila leo. Wakikumbwa na shida kiusalama, kijamii na hata kiuchumi.

Kutokana na wadadisi wa mambo, wafanya siasa walio madarakani tangu miaka, waonekana wenyi kuzingatia faida zao, wakitupilia mbali hitaji za raia. Wamoja miongoni mwao hufunga safari kwenda ugenini wakati wa likizo. Nakuonekana wengi kwenyi majimbo kuhamasisha raia wakati huu wa uchaguzi.

Wamoja tulio wahoji kuhusu ziara walizozifanya muda wa mhula wao, wengi wasema kuwa hawakupata muda ya kuona raia, wakihakikisha kwamba wapo bungeni ama madarakani kupitia pesa walizozitowa kwa raia muda wa kampeni. Hawa waendelea mara tena kusii raia wawachaguwe, Ingawa kuna wale ambao ni mara ya kwanza kugombea uchaguzi.

Waliokuwa madarakani waendelea kuahidi kwamba wataboresha maisha ya raia. Ijapo walitolewa muda wa kutosha, ili kuleta mabadiliko kuhusu hali ya maisha ya raia. Wamoja miongoni mwao watowa matokeo ya uwongo kwa kujipendeza na kutaka wachaguliwe mara tena. Na baadae kumwanga pesa ambazo ni mali ya raia walizo pora miaka mingi.

Wale ambao ni mara ya kwanza kujitokeza waahidi kutumika zaidi kupita walio hitimisha mihula yao bila kufanya chochote kile ama bila kufaulu.

<< Raia wachukuwe kalamu nyekundu, wakisahisha na kujuwa akina nani wanao kubaliwa warudishwe bungeni ama kwenyi ngazi zingine zinazo husu uchaguzi. Kwa kuwa wale walijaribu kufanya kazi. Ingawa wengine wakionekana kusinzia ndani ya vikao bungeni, wengine kukula rushwa ili wawapendeze viongozi wao wa kisiasa, wakizarau matakwa ya raia. Raia hawa wajuwe vizuri ni akina nani walioishi pamoja katika hali ngumu, wakifanya kazi pamoja, wakiwa himiza katika hali ya umaskini, wakiwaonyesha moyo wa upendo bila unafiki>>, afasiria mfanya siasa huyu Dady Saleh, ambaye ni mgombea kwenyi bunge la taifa nchini DRC.

Akiongeza kwamba sheria ya DRC yamupa kila mkongomani fursa ya kujielekeza mbele ya raia, hata kama akiwa mwenyi kudanganya raia ama la. Akiomba raia kuwa makini wasije, wakanaswe mara tena ndani ya mitego ya wafanya siasa wenyi uwongo.

Tukumbushe kwamba wengi miongoni mwa raia wanena kwamba watachaguwa wale wataweza kuwapa pesa, vyakula, vinywaji na mavazi. wakisahau njaa ambamo waendelea kuishi kila leo. Wengine waahidi kupokea vitu hivyo pasipo kuwachagua kwa kuwa hawakufanya chochote kile.

Wandishi.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire