![IMG-20230808-WA0096(2).jpg](https://i0.wp.com/larondeinfo.com/wp-content/uploads/2023/08/IMG-20230808-WA00962.jpg?resize=678%2C381&ssl=1)
Akihojiwa na mwandishi habari wa la ronde info, mtaalam katika kilimo Injenia BYEKA MOLIGI MABANZE Patient anena kukerwa na hali mbovu ambamo waishi raia jimboni Kivu ya kusini kwa jumla, na wale wa wilaya ya SHABUNDA kwa peke, eneo lake la kuzaliwa. Ni kwamba ni muda kwake kijana huyu kuleta mcango.
Raia wangojea mcango wake BYEKA Patient mtoto wa mwami MOLIGI MABANZE Raymond ili kutekeleza maendeleo
Akiongeza kwamba alipata muda wa kufikiri mbele afanye siasa, kuhusu namna waliotangulia walifanya kazi na jisi ya kupata suluhu. BYEKA MOLIGI aomba raia wamuunge mkono na wachaguwe wafanya siasa wapya.
<<Nikipata bahati ya kuchaguliwa na raia wa SHABUNDA, nikifaulu, nitaweka mkazo kwa kazi za kilimo na malisho. Mimi kama mtu aliyefunzwa kilimo. Nitaweka mkazo pia kwa afya ya raia, usalama kimalisho na ujenzi wa barabara vijijini. SHABUNDA ambayo ni wilaya isiyo endelea Nitajihusisha na mambo matatu; kilimo, afya na maadibisho. Barabara itakapo jengwa, raia watapeleka kwa raisi mazao ya shamba kunako Soko. Watatembelewa na mashirika ambazo zitaweza wahudumia. Nitakapo chaguliwa nitajibu kwa mambo hayo matatu,>> ahakikisha, BYEKA MOLIGI.
Nazani raia watatulazimisha mpango yetu ya kazi. Ni kupitia hiyo ndio watatambua wamuchague nani na nani waache. Wakichagua watoto wa nyumbani wanao wafahamu vizuri. BYEKA MOLIGI Patient angojea kuweka vikartasi vyake kwenyi Tume huru ya uchaguzi CENI, akiwa kandideti kwenyi bunge la jimbo Kivu ya kusini.
Yeye ni moja wapo wa wanamemba kwenyi shauri la vijana walega nchini DRC CJEL maarufu. << Mimi ni mwanzilishi wa Shauri la vijana walega nchini DRC CJEL maarufu,>>aeleza kijana huyu mfanya siasa. Akiwa pia muundaji wa kazi akiwa na jumba kadhaa kwenyi jimbo kadhaa za DRC. Anatengeneza pia chakula kutoka mazao ya shamba. Bila kusahau ufugo wa ngombe, mbuzi, nguruwe na kadhalika.
Juvénal Murhula.
Poster un Commentaire
Vous devez vous connecter pour publier un commentaire.