Prezidenti wa muungano wa soko mjini Bukavu Étienne Buhendwa anena kuunga mkono Raisi wa DRC Félix Antoine Tshisekedi TSHILOMBO, anayejitahidi usiku na mchana, ili kutekeleza usalama Kivu ya kaskazini. Ijapo wengi hawafahamu umuhimu wa uongozi wa kijeshi, wakisema kwamba matokeo si bora.
<<Mimi ninavulia kofia Raisi wa nchi, kwa kuruhusu uongozi wa kijeshi jimboni Kivu ya kaskazini, ambako matunda ni mazuri kwa sasa. Ingawa watu wengi huendelea kupinga matunda ya kazi hiyo, Raisi anafahamu mwenyewe kazi anayoifanya, Na ni yeye ataamua kukomeshwa kwa uongozi huo ama la, >>anena Étienne Buhendwa.
Akihojiwa kuhusu usalama mdogo, mauaji na utekaji nyara vinavyo ripotiwa kila leo Kivu ya kaskazini, Prezidenti wa muungano wa soko mjini Bukavu anena kwamba hali hiyo yaripotiwa hata kwenyi nchi zingine ulimwenguni, siyo Kivu ya kaskazini peke.
Kiongozi huyo aligusia hali ya soko mjini Bukavu ambazo zinahitaji kujengwa kwa jumla. Akitowa mfano wa soko Limanga ambayo inashambuliwa na waporaji, ila liwali aliahidi suluhisho kwa swala hilo. Pamoja na hayo soko kuu ya Kadutu, ambayo vyoo vinajengwa kwa msaada wake waziri husika na bajeti Aimé Bodji. Na soko zingine zitajengwa kwa msaada wa mke wa Raisi pamoja na liwali wa jimbo. Akiomba raia kutulia kwa kuwa kazi hizo zitatekelezwa na wahusika punde si punde.
Kwa wale wazani kwamba kazi hizo zinafanyika katika lengo la kufanya kampeni, Étienne Buhendwa anena kwamba ni jukumu la viongozi kufanya kazi kama desturi, pasipo kufikiri kuhusu kampeni. Akitowa mfano wa baba mwenyi jukumu la kulisha watoto wake, kuwajengea nyumba na kadhalika. Étienne afasiria kwamba baba huyu anapo hudumia watoto wake ni kawaida, ni jukumu lake, ila hatarajiye chochote kile.
Juvénal Murhula.
Poster un Commentaire
Vous devez vous connecter pour publier un commentaire.