Kivu ya kusini : Patient BYEKA MOLIGI aomba raia wa SHABUNDA kumuunga mkono ajili ya maendeleo

Akiondoka kwenyi chama cha kisiasa ANCE chake Norbert Basengezi, na sasa apatikana ndani ya chama ADRP chake François Masumbuko Rubota. Si mwengine, ni Patient BYEKA mtoto wa Mwami MOLIGI MABANZE Raymond wa usultani wa Wakabango ya kwanza, wilayani SHABUNDA. Mtaalam katika sekta ya kilimo, Patient BYEKA aliondoka ndani ya chama cha kisiasa ANCE kwa sababu zake binafsi. Atafanya yote iwezekanayo ili kutekeleza maendeleo pa SHABUNDA, eneo la kuzaliwa na hata Kivu ya kusini kwa jumla. Akiomba raia kutumika bega kwa bega.

Alinena hayo mbele ya ripota wa la ronde info, baada ya kuweka vikartasi kwenyi Tume huru ya uchaguzi CENI kwa kugombea uchaguzi jimboni Kivu ya kusini. << Nimeondoka ndani ya chama cha kisiasa ANCE, nikiwa na sababu zangu binafsi. Hali ya siasa hubadilika kila mara. Chama cha kisiasa siyo kanisa ambamo watu waweza kudumu. Pamoja na hayo, nimejibu kwa matakwa ya raia, nikiwa mtumishi wao. Nitaendelea kuwatumikia, kwa kuwa watanituma bungeni hapa karibuni, afasiria kijana BYEKA mwenyi umri wa miaka zaidi ya thelesani.

Usiku kama mchana apigana ajili ya maendeleo ya SHABUNDA, kupitia shirika FOMOKA lililopewa jina la babu yake, ambaye ni Sultani mkuu wa usultani wa Wakabango ya kwanza.<< Shirika lisilo la kiserkali FOMOKA lahusika na kuhamasisha raia mlango kwa mlango, likiwa na desturi: << KAZI NI KAZI>>. Jengo kubwa za tofali, kazi za shamba za vikundi zimetekelezwa kupitia shirika hilo. Na kutowa misaada, muungano wa afya. Bila kusahau shirika la hakiba na mikopo ya wanavijiji AVEC kwa lugha la kimombo>> anena kijana huyu mfanya siasa pia husika maendeleo.

Hakusahau kazi za kilimo, ufugo, hata ufugo wa samaki na kazi za mikono. <<Tunahamasisha pia raia kuhusu mila za walega. Samahani ya mila ya walega kupitia kupitia muungano : Mulega Muntu Umozi yaani Mulega ni mtu moja kwa kifupi MMU>>, aeleza Patient BYEKA kandideti kwenyi bunge la jimbo Kivu ya kusini.

Kuhusu usalama, kada huyu wa chama cha kisiasa ADRP anena kwamba shirika FOMOKA laandaa kila mara kazi za uhamasishaji dhidi ya vijana ili wasiingie ndani ya kundi zenyi kumiliki silaha. Kwa kuunda kazi za mikono, mafunzo kuhusu uraia, kubadili tabia, kupiganisha umaskini na kadhalika.

Kwa nini kutia mkazo kwake Patient BYEKA MOLIGI ?

Yeye ni moja wapo miongoni mwa wanaojitahidi kuhusu maendeleo wilayani SHABUNDA, na jimboni Kivu ya kusini kwa jumla. Kupitia kazi zake na hata ujuzi. Akiwa kijana mwenyi kuwa karibu na raia wakati wowote ule, mtetezi na kadhalika. Akisii raia kuweka vijana wanao wapenda nawo madarakani.

Tufahamishe kwamba Bwana Patient BYEKA anao mpango pia wa kukomesha uchukuzi kimagendo angani wa madini. Jambo linalo kwamisha maendeleo pa SHABUNDA. Akiwa na nia wilaya hiyo iweze kupata faida kupitia madini yake.

Juvénal Murhula.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire