Goma: Shida ni nyingi SHAKO TCHOMBA Souverain aomba raia kuwa makini kutochaguwa yeyote yule

Bwana SHAKO TCHOMBA Souverain ambaye ni mwanzilishi wa shirika la kufunza gari kwa jina la AUTO ÉCOLE VISiON 2008 na mwalimu mkuu kiufundi, aamuwa kama ilivyo kuwa hitaji yake hapo mbeleni, kwenda kutetea raia kwenyi tabaka za juu. Akiwa moja wa viongozi ndani ya kata Virunga, huyu apambana na usalama mdogo kila, leo ndani ya kata. Akijihusisha pia na maendeleo miaka chungu tele. Ijapo kutofikia lengo.

Kiongozi SHAKO TCHOMBA anena hayo akihojiwa na wandishi habari mjini Goma, mji mkuu wa Kivu ya kaskazini. Akifasiria hali kiusalama na kimaendeleo ndani ya kata Virunga, na mtaani Karisimbi kwa jumla.

<<Shida ya kwanza inayokumba kata yetu kwa jumla ni usalama mdogo. Tangu mwaka 2006, usalama mdogo umeonekana. Na kama hakuna utashi mwema wa viongozi utaendelea. Watu hushambuliwa kila leo, usiku sawa vile mchana, wakitatizwa na jambazi. Inabidi viongozi watafute suluhu kuhusu hayo. Watu kadhaa hupigania madaraka. Wanapo pata fursa ya kuongoza wanashindwa. Ndio maana raia wawe makini, wakijuwa ni akina nani watumishi wao kamili, wanaofaa na wa kila siku, >>afasiria Bwana SHAKO TCHOMBA.

Akiomba viongozi husika na usalama kutumika vilivyo, ili kutekeleza amani. Kwa viongozi wa tabaka za juu aomba uhusiano na wale wa tabaka za chini kuboresha kazi

Kuhusu maendeleo, Bwana SHAKO TCHOMBA ambaye ni mgombea uchaguzi kwenyi shauri la mtaa, anena kwamba eneo analoliongoza lakumbwa na matatizo chungu tele. Maji ya mvua kujaa nafasi nyingi, ukosefu wa jalala, kufungwa kwa njia ndani ya kata na kadhalika. Akikumbusha raia kuwa macho kwenyi uchaguzi wa mwezi disemba 2023.

Akiwa pia wa chama cha kisiasa LDG TCHOMBA anena kwamba ni mwito kwake kuanzisha shirika la kufunza watu gari AUTO ÉCOLE VISiON 2008 na hata kufanya siasa. << Nilikuwa siku nyingi nikikataa uongozi ndani ya kata. Nilijikuta nimeji orodhesha ndani ya shirika la kutetea haki ya binaadam ASVOCO . Baadae ndani ya chama cha kisiasa kilicho kuwa na lengo moja na shirika ASVOCO: Ndani ya chama, niliongoza vijana wa kata Virunga. Nikijihusisha na usalama. Hiyo ilipelekea nichaguliwe sawa kiongozi wa nyumba kumi mwaka 2006, kiongozi makamu wa avenue Muteberwa mwaka 2009, kiongozi wa avenue hiyo mwaka 2012. Tukiwa katani Virunga. Tunakumbwa na shida nyingi ndani ya kazi, ambayo haina mshahara, ila ni kujitowa. Kwangu ni mda wa kutetea raia kwa tabaka za juu,>> akomesha matamshi yake

Juvénal Murhula.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire