Kivu ya kaskazini : Promesse KAMBALE MATOFALI atetea raia kuhusu hali mbovu waishimo kila leo

Mwanabunge jimboni Kivu ya kaskazini, ambaye kwa sasa mgombea uchaguzi kwenyi bunge la taifa Promesse MATOFALI ni moja wapo miongoni mwa wanabunge, walioonekana kujitowa ili kutetea raia muda wa mhula wao kwenyi bunge la jimbo Kivu ya kaskazini.

Katika uchunguzi ulioendeshwa na gazeti la ronde info, mwanabunge huyu Promesse MATOFALI ambaye ni mgombea uchaguzi kwenyi bunge la taifa nambari 146 alijihusisha na kazi nyingi akiwa mwanabunge wa jimbo Kivu ya kaskazini.

Mfano kuomba ivunjwe kwenyi bunge la taifa, sheria inayohusu uraia, ikiwa ni namna ya kuwatenga wakandideti wengine kwenyi uchaguzi mwaka 2023. Promesse MATOFALI alinena pia kuhusu uhaba wa dawa yaani serum ndani ya jumba kadhaa mjini kutokana na kupandishwa kwa ushuru . Ikiwa matatizo kwa wagonjwa.

Akitowa kauli kuhusu kupanda kwa mafuta ya petroli mjini Goma. Na hii ni moja wapo miongoni mwa shida zinazokumba raia mjini. Mwanabunge huyu alilaumu matumizi mabaya ya bajeti mwaka 2020 naye liwali wa jimbo. Akiwa na mashaka kuhusu mwaka 2021, kwa kuwa mwaka 2020 haikufaulu.

Mchaguliwa wa Butembo Promesse MATOFALI alionyesha kwamba uongozi wa kijeshi haikufaulu kutokana na usalama mdogo unaendelea kutanda Kivu ya kaskazini na Ituri. Nawo raia wakipinga uongozi huo Huyu aliweka kwenyi bunge la jimbo, mradi wa sheria kuhusu kukinga na kuinua haki za vijana. Namna ya kusaidia vijana kuunda kazi na kadhalika Akitetea pia wazazi kuhusu kupandishwa kwa malipo ya shule la sita la sekondari toka dola 50 za marekani hadi dola 70 za marekani.

Mwanabunge Promesse MATOFALI wa chama cha kisiasa Ensemble pour la République chake Moïse Katumbi alikuwa miongoni mwa wanabunge wa upinzani, wakiomba liwali wa jimbo kutowa mafasirio kuhusu matumizi ya dola milioni 15 za marekani na kadhalika.

Hayo ni machache miongoni mwa kazi alizoendelea kuzitekeleza mwanabunge wa jimbo Kivu ya kaskazini Promesse MATOFALI , ambaye kwa sasa atagombea uchaguzi kwenyi bunge la taifa nambari 146.

Juvénal Murhula.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire