Akihojiwa na wandishi habari mjini Goma kuhusu kampeni ya uchaguzi, Profesa Joseph Kitaganya ambaye ni kandideti kwenyi bunge la jimbo Kivu ya kaskazini nambari 171 anena kukerwa na tabia ya wakandideti wamoja ambao wanatumia watu ili kuharibu na kuondowa picha za kandideti wengine. Yeye akiwa mhanga wa vitendo hivyo vya kinyama, kando ya shule la ellmu ya juu ISC, siyo mbali pia na shule la sekondari INSTIGO.
<< Mtu ambaye hakufunzwa na jamaa, hakuna mahali pengine ataweza kufunzwa. Hawa ni wahuni ambao wanafanya vitendo hivyo. Mimi mwenyewe nilikuwa mhanga wa vitendo hivyo vya kinyama. Picha yangu iliondolewa kando ya shule la elimu ya juu ISC, si mbali pia na shule la sekondari INSTIGO. Wahuni hawa waonekana kutumwa na wenzetu makandideti ambao tayari wamekuwa na woga. Wakandideti hawa waache mwenyi kufaulu aweze kufaulu, akinena kwa Joseph Kitaganya kandideti kwenyi bunge la jimbo Kivu ya kaskazini.
Akisema kwamba hatavunjika moyo, ataendelea na vita, akiweka picha zingine hadi kufikia lengo. Kandideti huyu alaumu hali ya makandideti hawa wenyi nia mbaya, wamoja walio pora mali ya serkali ndio wajaza picha mji mzima. Ila ahaidi kwamba, ingawa anakwenda bungeni siyo kwa kuiba, ila kufanya kazi.
Kandideti kwenyi bunge la jimbo Joseph Kitaganya asema kushangaa kwa kuwa wanabunge wamoja humaliza mhula pasipo kutetea raia, ijapo ndio kazi iliwapeleka bungeni. Wamoja miongoni mwao hawajuwe jukumu lao. Hawa waahidi ujenzi wa shule, vilalo, barabara, hospitali na kadhalika. Ndipo aomba raia wamuchague akiwa nambari 171, kwa kuwa hatatoka kwenyi msimamo wake. Atajitahidi kupanza kuhusu shida za wachaguzi wake.
Juvénal Murhula.
Poster un Commentaire
Vous devez vous connecter pour publier un commentaire.