Kivu ya kaskazini : Bunge la watoto jimboni humo laendelea kutetea haki ya mtoto

Bunge la watoto jimboni Kivu ya kaskazini lasema kuhusu ukiukaji wa haki ya watoto jimboni humo. Hiyo ni kutokana na hali ya vita ambamo waishi watoto. Hasa wale wenyi kuishi katika hali mbovu ndani ya kempi, wakiwa wahami wa vita, pamoja na wazazi wao. Pamoja na vingine vitendo vyenyi kukiuka haki ya mtoto.

Alinena hayo Kiongozi wa bunge la watoto jimboni Kivu ya kaskazini IMANI KADUKU , ajili ya kusherekea siku ulimwenguni kuhusu haki ya mtoto, inayosherekewa tarehe 20 novemba kila mwaka.

Katika kikao na wandishi habari, Kiongozi wa bunge la watoto jimboni Kivu ya kaskazini alinena kujihusisha pia na haki ya watoto wanaoorodheshwa ndani ya kundi zenyi kumiliki silaha. Akitowa tahazari kwa kundi hizo kuto orodhesha watoto, kwa kuwa nafasi yao ni kwenyi shule.

Pamoja na hayo akitowa angalisho kwa wale watakao tumikisha watoto katika kampeni ya uchaguzi ambayo imeanza hii tarehe 19 novemba nchini DRC. Watoto hawa hawastahili kufanya siasa, sheria ikiwakataza.

Prizidenti wa bunge la watoto jimboni IMANI KADUKU asema kwamba watoto wafunzwa kila mara kuhusu zao, na kwamba wengi miongoni mwao wamekwisha kufahamu mengi kuhusu haki zao, kwa kuwa wamepata mafunzo kamili

Juvénal Murhula.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire