Kivu ya kaskazini : Moïse Katumbi aahidi kuboresha maisha ya wakongomani mbele ya umati uliompokea kwa shangwe na vigelegele

Akiwasili mjini Goma kiisha mchana kati, kandideti kwenyi uraisi wa taifa Moïse Katumbi nambari 3 amepokelewa kwa shangwe na vigelegele na umati kwenyi uwanja wa ndege. Ni katika hali hiyo ndipo alisindikizwa kwenyi uwanja wa kandanda AFIA ambako alihotubia raia waliokuwa wengi kwa kumlaki.

Muda wa saa na nusu, kandideti kwenyi uraisi Moïse Katumbi aligusia mambo mengi, hasa hali waishimo raia jimboni Kivu ya kaskazini. Alisema kwamba atafanya yote iwezekanayo ili kumaliza vita jimboni Kivu ya kaskazini. Aliahidi pia kuboresha hali ya kijamii ya raia na vijana waweze kupata kazi.

Kandideti kwenyi uraisi Moïse Katumbi ameahidi kulipa mishahara mizuri kwa wafanya kazi wa serkali, yaani walimu, waganga, askari jeshi na askari polisi. Alisema tena ataleta suluhu kwa shida ya umeme na maji. Akisisitiza kukomesha vita ya M23 ambayo inatatiza raia miaka chungu télé jimboni Kivu ya kaskazini.

Kandideti Raisi Moïse Katumbi alisema ataweka bajeti maalum kwenyi majimbo ya Kivu ya kaskazini na Ifuri. Aliahidi miliardi tano kwenyi majimbo hizo mawili ili ya kuboresha maisha ya raia wa majimbo hayo mawili ambayo imeteketea.

Moïse Katumbi amesema kwamba ni miaka mingi amezuwiliwa kuzunguka nchini, ila muda umefika kwake kwa kugombowa nchi ndani ya utumwa. Huyu alisema kwamba yeye si Raisi wa kulialia, kama ilivyo kwa wengine.

Pamoja na hayo alisema atatembelea wahami ndani ya kempi ya Kanyaruchinya, ili ya kuweza kuwahudumia, kwa kuwa anakerwa na hali ya mateso ambayo wanaiishi.

Juvénal Murhula.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire