Goma: Wachuuzi wa soko ya Ndosho waahidi kuwachagua wanabunge Josué MUFULA na HAMISI MWANZA

Wanabunge hawa Josué MUFULA pamoja naye HAMISI MWANZA wamepokelewa hii ijumaa tarehe 2 disemba kwa shangwe na vigelegele na ma mia ya wachuuzi wa soko ya Ndosho. Wakiahidi kwamba watachagua wanabunge hawa wawili kutokana na kazi nzuri walizo zitekeleza wakati wa mhula wao bungeni.

Hiyo ilitamkwa wakati wa sherehe ya kuzinduwa bomba ya maji iliyojengwa kwa msaada ya mwanabunge Josué MUFULA akitembea pamoja naye HAMISI MWANZA kandideti kwenyi bunge la taifa tarafani Nyiragongo.

Mbele ya yote, prezidenti wa kamati ya soko hiyo pamoja na akina mama wachuuzi anao waongoza,  walishukuru waalikwa wawo, wakiwapigia aksanti kwa kuwa walikumbwa siku nyingi na matatizo, ila hawakujuwa wamuliliye akina nani. Akisema kwamba ni namna ya viongozi hawo kuwa panguza machozi.

Viongozi hawa walipokea tuzo mbali mbali toka wachuuzi hawo, yaani vyakula, picha, alama ya mapendo mbele ya viongozi hawo, wakizungukwa na idadi kubwa ya wachuuzi kwenyi soko hiyo.

Mbele ya kuanza kipindi cha uzinduzi, mwanabunge wa taifa HAMISI MWANZA alisema kumusindikiza mwenziwe Josué MUFULA kwa kazi ya uzinduzi wa bomba ya maji. Akiomba raia kuchaguwa kandideti kwenyi uraisi nambari 20, Raisi Félix Antoine TSHISEKEDI, ambaye alionyesha wazi kwamba DRC inapigwa vita na nchi ya Rwanda. Na kuomba raia wasisahau nambari 23, 58 na mabunge wao wengine, wa majimbo na hata wale wa mitaa.

Upande wake, mwanabunge Josué MUFULA kandideti kwenyi bunge la taifa nambari 58 alieleza kwamba raia wa soko hiyo hatakumbwa tena na shida ya maji. Akisema kwamba raia watashota maji usiku kama vile mchana. Mwanabunge ameeleza kazi  nyingi za mikopo kwa akina mama wengi mjini Goma, ili ya kuwarahisis hia chakula cha kila leo kwa jamaa na mengineo. Akina mama walio wengi wakihakikisha matamshi yake mwanabunge Josué MUFULA.  MUFULA ambaye ni nambari 58 aliahidi  kuendelea kupigana pia juu ya usalama wa jimbo, akitaja visa vya watu ambao amekwisha wahudumia katika hali ya usalama, pia kuhudumia vijana kwa shule . Akiomba raia kuchaguwa kandideti kwenyi uraisi nambari 20, Félix Antoine TSHISEKEDI TSHILOMBO, Yeye akiwa nambari 58 kwenyi bunge la taifa, HAMISI MWANZA nambari 23 kwenyi bunge la taifa pia, pamoja na wanabunge wengine jimboni na hata mitaani.

Kipindi cha uzinduzi wa  bomba hiyo kilikuja baadae, mbele waalikwa kunyatuka wakisindikizwa na umati ukiimba kwa furaha, shangwe na vigelegele.

Juvénal Murhula.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire