Kivu ya kaskazini : Redio na televisheni ya taifa RTNC imeshimika rasmi kiongozi mpya Bwana Tuver Hundi

Sherehe za kubadili madaraka zilifanyika hii ijumaa tarehe 15 disemba 2023, mbele ya ujumbe wa RTNC kutoka mjini Kinshasa, wapasha habari wa kituo hicho mjini Goma na wandishi habari wengine wengi mjini, bila kusahau ndugu na marafiki.

Kiongozi mpya wa Redio na televisheni ya taifa RTNC Tuver Hundi ni mwandishi habari mwenyi ujuzi, ambaye ametumika miaka chungu tele, kwenyi kituo hicho RTNC mjini Goma.

Akichukuwa kauli wakati wa sherehe, Tuver Hundi aliahidi kwamba atafanya Redio na televisheni ya taifa RTNC kuwa mfano bora wa kuiga. Pamoja n’a hayo, ataboresha kazi kulingana na maswala za amani na zile za usalama.

Wadadisi wa mambo wazani kwamba Redio na televisheni ya taifa RTNC, imepata bahati kupitia mjuzi huyu katika upashaji habari , ambaye atatumika zaidi kwa manufaa ya raia.

Juvénal Murhula.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire