DRC : TSHISEKEDI TSHILOMBO Félix Antoine anena kuwa mwenyi furaha kwa kumcagua kwa mhula wa pili

Akila kiapo kwenyi uwanja wa kandanda Martyr de la Pentecôte mjini Kinshasa, hii ijumaa tarehe 20 januari 2024 Raisi wa taifa TSHISEKEDI TSHILOMBO Félix Antoine aahidi raia kutekeleza usalama mashariki mwa DRC, kukomesha ukosefu wa kazi hasa kwa vijana, pesa za kongo kupata samani, kuinua uchumi na kadhalika.

Aliahidi hayo wakati wa sherehe za kula kiapo mbele ya korti ya sheria, na maraisi wengine na hâta wajumbe wa ma raisi wengine kutoka nchi za ugenini. Bila kusahau umati wa wakongomani.

<<Nashukuru makandideti Raisi walioacha kugombea ili nipate kufaulu, wanamemba wa shirika la raia na wengine wote walioruhusu nipate kuchaguliwa mara tena. Ninayo moyo wa shukrani kwa wote. Wanainchi wapenzi, nafahamu matakwa yenu yaani munakumbwa n’a ukosefu wa kazi hasa kwa vijana, kujigemea kwa mwanamke, ukingo wa watu walemavu na wengine wote wasiojiweza>> anena Raisi akihotubia umati wa wakongomani.

Aliahidi pia kwamba pesa za kongo zitakuwa na samani, kuinua uchumi ili kutotegemea bidhaa toka nje. Pamoja na hayo kukomesha hali ya usalama mdogo inayosababishwa na magaidi wa kila aina, na kukinga raia na mali yao. Akisisitiza kukomesha hali ya vita inayokumba DRC miaka chungu tele.

Kuhusu maendeleo, kutekeleza mradi 145 territoires yaani maendeleo dhidi ya wilaya 145 nchini DRC. Pamoja na hayo shule kwa bure, na kuboresha sekta ya afya ili wakongomani wapate kufikia matunzo bora na kadhalika.

Juvénal Murhula.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire