DRC:  Tshisekedi Tshilombo Félix Antoine anena kuwa mwenyi furaha kwa kumchagua kwa mhula wa pili

Akila kiapo kwenyi uwanja wa kandanda Martyr mjini Kinshasa hii ijumaa tarehe tarehe 20 januari , Raisi wa taifa Tshisekedi Tshilombo Félix Antoine aahidi raia kutekeleza usalama mashariki mwa DRC akiahidi vijana kukomesha ukosefu wa kazi, pesa za kongo kuwa na samani, kuinua uchumi na kadhalika.

Raisi wa DRC TSHISEKEDI TSHILOMBO Félix Antoine aliahidi hayo wakati wa sherehe za kula kiapo mjini Kinshasa mbele ya korti ya sheria, ma raisi wengine wengi pamoja wajumbe wa ma Raisi wengine toka nchi za ugenini, bila kusahau umati wa wakongomani.

<<Nashukuru makandideti  Raisi walioacha kugombea ili nipate kufaulu, wanamemba wa shirika la raia na wengine wote walioruhusu nipate kuchaguliwa mara tena. Ninayo moyo wa shukrani kwa wote.  Wanainchi wapenzi, nafahamu matakwa yenu, yaani munakumbwa n’a ukosefu wa kazi, hasa kwa vijana, mwanamke kujitegemea, ukingo wa watu walemavu na wengine wote wasiojiweza,>> anena Raisi akihotubia umati

Aliahidi pesa za kongo kuwa zenyi samani, kuinua uchumi ili ya kutotegemea bidhaa toka nje.

Pamoja na hayo kukomesha hali ya usalama mdogo, inayosababishwa na magaidi wa kila aina, na kukinga raia na mali yao. Akisisitiza kukomesha hali ya vita inayokumba DRC miaka chungu tele.

Kuhusu maendeleo, kutekeleza mradi 145 territoires yaani maendeleo dhidi ya wilaya 145 nchini DRC,

Pamoja na hayo shule kwa bure, na kuboresha sekta ya afya ili wakongomani wapate kufikia matunzo bora na kadhalika.

Juvénal Murhula.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire