Mtu mioja kujerehiwa, barabara kadhaa karibuni zaoneka karibu wazi, basi na teksi zikitembea peke tnngu saa za asubui. Watu wengi wakitembea kwa migulu barabarani. Wengine kwenyi mashanganjia wakikosa namna ya kujielekeza kazini na mahali pengine. Hali ikipunguza pua msongamano barabarani kama ilivyo desturi.
Hali hiyo ilionekana tangu asubui ya juma tatu tarehe 29 januari 2024 mjini Goma mji mkuu wa jimbo la Kivu ya kaskazini
Duru za karibu na shirika la waendesha pikipiki mjini Goma hawa wapinga iliochukuliwa viongozi wa jimbo. Inayokataza waendesha pikipiki kutembea nyuma ya saa kumi na mbili ya jioni. Na atakaye naswa ataazibiwa vikali
Duru zingine toka upande wa Majengo zaeleza kwamba mwanafunzi moja aliyetoka shuleni, amejeruhiwa eneo hilo kutokana na risasi iliyofyatuliwa na askari polisi wakati wa hekaheka .Askari polisi hawa wakionekana kwenyi mashanganjia nyingi mjini Goma tangu alfadjiri.
Tufahamishe kwamba, ni tangu siku nyingi wizi waonekana kupanda kiasi mjini Goma na kandondo. Watembeza pikipiki kadhaa wakizaniwa kujihusisha na vitendo hivyo haramu. Ndipo viongozi jimboni kuchukua hatua ili kutaka kujua kinaganaga chanzo cha maovu hayo.
Kwa sasa, hali imeanza kuwa tulivu tofauti na alfadjiri.
Juvénal Murhula.
Poster un Commentaire
Vous devez vous connecter pour publier un commentaire.