Kivu ya kaskazini: Muungano kwa jina la Maarifa unalenga ujenzi wa uchumi DRC, ambao watembea sambamba na usalama

Exif_JPEG_420

Akihojiwa na wandishi habari baada ya kikao, John TSONGO moja wa memba wa Muungano kwa jina Maarifa aomba raïa jimboni Kivu ya kaskazini kusapoti vijana mjini Goma na jimboni Kivu ya kaskazini, ili waweze kununua bidhaa, katika lengo la kutengeneza vitu vinavyo hitajika. Wakitumia akili na ujuzi, ili sote tuhuzurie kwenyi ujenzi wa uchumi ulio timamu. Nchi yetu DRC ipatikane miongoni mwa nchi bingwa kati ya nchi zote za kimataifa. Muungano Maarifa wazani kwamba yatawezekana.

Bwana John TSONGO anena hayo baada ya kikao iliyojumwisha wanamemba wa Muungano Maarifa, wakiwa wafanya biashara, waendesha ajira katika mipango kadhaa ya kuendesha miundo mbinu ili kuchangia kwenyi ujenzi wa uchumi nchini DRC.

Ilikuwa hîi juma mosi tarehe 16 februari 2024 mjini Goma. << Maarifa ni kusema ujuzi. Kwa ngambo yetu, Maarifa ina maana incubateur katika lugha la kimombo. Incubateur d’entreprise kwa lugha la kimombo inamanisha kwamba sisi sote tunawahimiza wafanya biashara, waendesha ajira katika mipango mbali mbali ya kuendesha miundo mbinu yao, ili kuchangia ndani ya ujenzi wa uchumi nchini DRC,>> afasiria mwanamemba huyo.

John TSONGO asema kwamba wengi kati ya waendesha ajira hawo ni vijana ambayo hawana fursa ya kutosha ili kuendesha uchumi kama inavyofaa, wakijaribu kila moja wao kwa ngambo yake, kuhusu pato ndogo, wakitafuta kuendelea, wakitumikisha wengine, wote pamoja wachangie kwa mkopo kiwango fulani katika lengo la kuhuzuria kwa ujenzi wa nchi.

<<Kikao ya leo ilihusu waendesha ajira hawo. Wengi miongoni mwao waliorodheshwa mwezi disemba mwaka 2023. Wakinena kuwa tayari kwenyi kikao ya vionyesho yaani foire kwa lugha la kimombo, ambayo tunaandaa mjini Goma tariki 15 hadi 16 machi ikiwa ijumaa na juma mosi, kwenyi Full gospel,>> anena huyu memba wa Muungano Maarifa.

Wakati huo vijana waendesha ajira kuonyesha vitu wanavyo vitengeneza kwa kutumia akili kwa namna yao wenyewe. Hapo watapatikana wanaojenga vyombo vya kusaga mahindi yaani moulin, kwa jumla wale wenyi kutengeneza vyombo mbali mbali, vinywaji kutoka matunda, wanaoshona mavazi. Kutapatikana vitu vya kuvutia ambavyo wakaazi watavitizama. Hawa watakuja kununua, namna ya kusapoti uchumi nchini, afasiria John TSONGO.

Akiongeza kwamba Muungano Maarifa watumika bega kwa bega na serkali, ukiwa na vikartasi halali vinavyo ruhusu kufanya kazi yake. Na kwamba viongozi wa tabaka zote, usalama hata administration wamefahamishwa kuhusu kikao hicho mwezi machi. Na kwamba Muungano Maarifa unashirikiana hata na shirika zingine za serkali nchini DRC ; mfano FPI,  OCC na kadhalika.

John TSONGO moja wa memba wa Muungano huu anena kwamba ingawa wamoja ni Wazalendo kiusalama, wao ni Wazalendo kiuchumi. Na ndio mada ya kikao  ; uzalendo kiuchumi. Na kusema kwamba sisi sote tuwe Wazalendo kwa kutafuta usalama. Tukiweka nguvu zetu pamoja, ili tupate kuhuzuria ujenzi wa nchi, ngambo ya usalama na ngambo ya uchumi.

Akijibu kuhusu namna wahudumia waendesha ajira na wafanya biashara humu jimboni ijapo usalama mdogo kiasi, huyu anena kwamba hiyo ni shida kubwa.<< Jambo moja ambalo watu wapashwa fahamu; uchumi una haja ya usalama. Ili usalama uboreshwe inabidi pesa zipatikane, uchumi itekelezwe. Ni kusema kwamba uchumi unajengwa kutokana na askari polisi na jeshi. Ili vyote wiwe timamu inabidi pesa. Kwa mafasirio mengine, hakuna pesa ingawa hakuna uchumi. Vikosi vya usalama ama jeshi havitapata fursa ya kuleta usalama. Upande mwengine, waendesha ajira na wale wa viwanda hawatapata namna ya kutumika kama hakuna usalama. Vyote vyaambatana na viboreke ili nchi isonge mbele. Akitaja vitu vitatu vinavyo pelekea nchi ulimwenguni kusonga mbele, yaani usalama, uchumi na hata diplomasia. Na ndio maana tunalo lengo la kusindikiza DRC katika sekta hiyo ya uchumi,>> akikomesha matamshi yake John TSONGO moja wa memba wa Muungano Maarifa.

Juvénal Murhula.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire