Goma : Shirika lisilo la kiserkali PROJUSTICIA lahusika na haki ya binaadam, hasa kwa akina mama wahami waliobakwa

Shirika kwa jina la PROJUSTICIA liliandaa mkutano na wandishi habari katika mradi Haki ya mwanamke jimboni Kivu ya kaskazini. Baada ya kuchunguza vitendo vya ubakaji anavyo avitendewa mwanamke mhami ndani ya kempi na kando kando. Hasa wakati anajielekeza mahali kadhaa ajili ya kutafuta namna ya kuishi. Hawa wanatendewa kila leo ubakaji na watu wenyi kumiliki silaha, wanapo jielekeza kwenyi shamba kutafuta kuni na hata chakula

Shirika lisilo la kiserkali PROJUSTICIA kupitia mwanasheria Justin Mushoko laonyesha visa vingi vya ujeuri na hata ubakaji waliyo itendewa akina mama, hasa wahami waishio jimboni Kivu ya kaskazini na hata Ituri mashariki mwa DRC.

Shirika hili likikerwa ndipo liliamua kutumika bega kwa bega na vyombo vya sheria nchini DRC, tangu miaka tatu sasa. Ni katika lengo la kufunza raia kuhusu kupitia mada zinazohusu sheria na hasa haki ya binaadam. Kuelewesha raia hawa namna sheria inatumika, vizuizi anavyo vikuta  mkongomani anapotaka kutetea haki yake.

Kwake mwanasheria Justin Mushoko, ni ndizo lengo za kuunda shirika lisilo la kiserkali PROJUSTICIA na vijana wanasheria pamoja na wandishi habari kwenyi eneo. Pamoja na hayo kuanzisha rasmi namna ya kujitetea kwa wahanga wakijisikia kuwa huru kwa kutoa malalamiko wakati wanatendewa ujeuri.

Shirika lisilo la kiserkali PROJUSTICIA laomba kila yule wa moyo mwema kusapoti kazi hiyo, ili mwanamke ambaye anatoa maisha kwa kumzaa mtoto,  aweze kupewa haki yake. Kila mtu aweke mkono ndani ya mfuko wake akisindikiza wahanga wa ujeuri na ubakaji ili kuwapanguza machozi

Shirika hili likinena kwamba linakumbwa na shida kipesa, kutokana na mchango ndogo wanotumikisha.

Tufahamishe kwamba mashirika zenyi kutetea haki ya binaadam za kimataifa na hata za kitaifa zatowa idadi kubwa ya ubakaji wanayo itendewa wanawake wahami na hata watoto ndani ya kempi na kando kando. Shirika la kimataifa UNICEF likitoa visa elfu 38 vya ujeuri mwaka 2022. Tangu tarehe 17 hadi tarehe 30 aprili kundi ya waganga yaani MSF limetunza watu 674 wahanga wa ubakaji na kadhalika.

Juvénal Murhula.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire