Goma : Shirika lisilo la kiserkali kwa jina la Maarifa laanda kikao kuhusu kilimo na viwanda yaani foire agro industrielle kwa kimombo

Leo tulikutana na wafanya biashara pamoja na waendesha ajira, ili kutayarisha mkutano kuhusu kilimo na viwanda na kazi zingine za usani yaani foire agro industrielle kwa kimombo. Mkutano huo ni tarehe15 na 16 machi 2024 kwenyi jumba Full gospel mjini Goma. Tulipenda kujionea binafsi matunda ambayo waendesha ajira na hata wafanya biashara wataonyesha siku hiyo mbele ya umati. Na ndio kiini cha kukutana leo ili tutayarishe pamoja.

Matamshi hayo ni yake Bwana John KAVYAVU akiwa kiongozi tendaji na mwanzilishi wa Muungano usio wa kiserkali  Maarifa baada ya kutanana na waendesha ajira na wafanya biashara hîi juma nne tarehe 5 februari 2024 kwenyi jumba la wandishi habari UNPC mjini Goma.

Akisema kwamba wameshangaa kuona kazi mhimu ambazo wazitekeleza leo vijana wa Goma. <<Tulifurahishwa na vitu ambavyo vitatumiwa ndani ya mkutano huo kuhusu kilimo na viwanda, yaani foire agro industrielle kwa kimombo. Tulishangaa kuona vitu vingi ambavyo watoto wa Goma tayari wamevitengeneza. Hapo hapo tumeona viato, vinywaji vya kila aina, mfuko ya mkononi na kadhalika. Vitu hivyo ni vizuri, hatupashwi nunuwa tena hivyo vinavyo toka katika nchi za kigeni>>, anena kiongozi tendaji wa Muungano Maarifa Bwana John KAVYAVU.

Akihojiwa kuhusu tofauti kati ya kikao hiki kya sasa na vile vilifanyika hapo mbeleni, Bwana John KAVYAVU anena kwamba ni namna ya kuendelesha tu kazi.  Kazi tunazozifanya sisi Muungano Maarifa ni kuinuwa mazao zinazotengenezwa hapa nyumbani, na kuhamasisha raia kuhusu umuhimu wa kutumia vitu vya nyumbani. Kazi tunazoita uzalendo kiuchumi. Ni kusema kwamba unapotumika, pesa utakazo zipokea, uweze kununua vitu ambavyo vinatengenezwa hapa mjini kwetu, afasiria John KAVYAVU kiongozi tendaji wa Muungano Maarifa.

Akiongeza kwamba ukifanya hivyo, kwa kweli utakuwa umeleta mchango wako kuhusu maendeleo mjini. Akitowa mwangaza kwamba ingawa utaacha kununua vitu vya nyumbani, na kwenda kununua ugenini, kwa hiyo utakuwa mwenyi kuinua uchumi huko ugenini na kuacha ule wa nyumbani uzorote.

Akiomba raia kuja wenyewe kwani kuambiliwa kuna uongo.<< Tunaomba raia kuja wengi wakihamasisha wengine kwa tarehe 15 na 16 machi, ili kujionea binafsi mazao tunayo tengeneza kwetu mjini Goma. Na hata mazao zingine toka miji ya Butembo na hata ya Béni.>>aeleza kiongozi huyu.

John KAVYAVU aongeza kwamba kunaandaliwa siku hiyo tu mchezo wa kupima bahati yaani tombola. Kwa hiyo, watu watakao fika mapema nafasi hiyo, watapewa tickets, na hiyo itawapa fursa yakufaidia kitu kimoja; mfano jiko, vinywaji mbali mbali, sabuni na kadhalika. Vitu hivyo ni kwa faida ya watu watakao fika mapema kwenyi mkutano. Kazi zinaanza saa mbili asubui kuendelea mchana mzima.

Juvénal Murhula.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire