Kivu ya kaskazini : Raia wa Nzulo wapinga hatua yoyote kuhusu udongo wao ndani ya kikao yenye kuandaliwa na shirika ICCN na washiriki wengine

Sisi tunapatikana hapa. Tumesikia kwamba kuna watumishi wamoja wa shirika ICCN katika mbuga la kuhifadhi wanyama la Virunga pamoja na washiriki wengine, ambao wanaandaa kikao kuhusu udongo wa kijiji Nzulo. Wakitarajia kusahini makubaliano kuhusu udongo huo. Tunapochunguza tunaona kwamba hakuna mtu anaye wakilisha raia wa Nzulo na hata viongozi wa asili eneo hilo. Swali ni kwamba namna gani kuandaa kikao ambamo hawashirikishwe raia na hata viongozi wa asili wa mahali ? Ni miaka chungu tele shirika ICCN limevamia udongo wa Nzolu. Tulijielekeza kwenyi vyombo vya sheria, uamzi kwamba sisi wenyeji wa udongo.

Matamshi yake  Justin  KAKESA moja wa wakaazi wa Nzulo. wakiandamana mbele ya jumba la wandishi habari mjini Goma UNPC, ambamo mulifanyika mkutano huo wa shirika ICCN na washiriki wake.

Kwake mkaaji huyu, ni kundi la watu kwenyi shirika ICCN  ambao wadanganya wafadhili kwamba kunapatikana mizozo pa Nzulo, na kwamba  shirika ICCN ina  udongo mahali hapo.

<<Sisi tumeelewa kwamba ni namna ya watafanya kazi hawo kuendelea kupokonya pesa wakitumia mizozo upande wa mbuga la Virunga. Kwa kuwa watu hawo hawataki mizozo ikome eneo hilo. Na hîi tunapinga kabisa. Tunaangazia ulimwengu mzima kwamba hakuna mizozo pa Nzulo. Tunapatikana kwenyi udongo wetu,>> anena mkaaji huyu.

<<Hakuna mizozo pa Nzulo, sheria ya Kongo ameweka uamzi kuhusu haki yetu. Tunalaumu tabia ya wafanya kazi wamoja wa shirika ICCN, na wengine wanao washiriki, ambao wapata pesa kiasi, wakipitia mizozo na hata kila mizozo kando ya mbuga la kuhifadhi wanyama la Virunga. Ndio kila leo hukusanyika wakidanganya wafadhili, >>afasiria Bwana Justin KAKESA

Raia wa Nzulo waomba serkali kuazibu watu hawa wanaotaka kuangamiza maelfu ya watu pa Nzolu, eneo la  Kamuronza, usultani wa Bahunde wilayani Masisi  jimboni Kivu ya kaskazini.

Juvénal Murhula.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire