Goma: Muungano usio wa kiserkali Maarifa waalika raia kuja kujionea na kununua vitu vyenyi kutengenezwa nyumbani

Exif_JPEG_420

Muungano usio wa kiserkali Maarifa unaandaa mkutano kuhusu kilimo na viwanda tangu hîi ijumaa tarehe 15 hadi tarehe 16 machi mwaka huu kwenyi jumba Full gospel mjini Goma. Ni katika lengo la kuinua mazao inayotengenezwa mjini Goma kwa pekee na nchini DRC kwa jumla.

Matamshi yake kiongozi tendaji wa Muungano Maarifa John KAVYAVU wakati wa mkutano na wandishi habari kwenyi jumba UNPC mjini Goma.

<<Tunatumika pamoja na waundaji kazi ambawo wanatengeneza vitu vya nyumbani wakivigeuza hadi matumizi. Tunayo furaha kubwa kwa raia mjini Goma,  tukitia matumaini kwenu. Ili kutangaza habari hîi kuhusu mkutano wa  kilomo na viwanda, ambao ni mara ya kwanza, utaanza kesho ijumaa tarehe 15 hadi tarehe 16 machi majira ya saa mbili kamili.  Watu waje kuhuzuria. Watakaofika mapema watatolewa tiketi kuhusu tombola, itakayo wapa bahati ya kupata kitu moja miongoni mwa vifaa vinavyo tandikwa. Mbele tuliweza kutana na waundaji kazi, tukitowa mafunzo, tukigunduwa vitu vingi vya samani vyenyi kutengenezwa na watoto wa hapa mjini. Goma. Ni fursa ya nyinyi raia kuja kujionea. Naamini mutafurahishwa,>> anena kiongozi tendaji wa Muungano Maarifa John KAVYAVU.

Kwake kiongozi tendaji, mkutano huo ni mwanzo wa kazi ambazo zitaendeshwa ili kusindikiza watu hawo.  Wakisindikizwa kwanza na Muungano Maarifa, pili na kazi za serkali na mwisho na raia ambao ni watumiaji wa mazao ya waundaji  kazi.

Akiongeza kwamba  watu waje kutazama mazao hayo yenyi samani na hawatakuwa n’a haja ya kutumia mazao yenyi kutoka ugenini. Na kwamba tukitumia mazao ya nyumbani tutakuwa wenyi nguvu nchini mwetu,  na hîi itaweza kuinua  jamii. Kwa kuwa ni nguvu kwetu kufikisha habari inabidi nyinyi wandishi habari kutapanya habari hiyo.

Swala Kadhaa ziliulizwa moja kwa moja na wandishi habari.  Zikuhusu  maandalizi ya kikao wakati hali ya usalama yazorota jimboni,  zingine kuhusu uwingi na hâta uzuri wa mazao, uhusiano kati Muungano Maarifa na kazi za serkali ili kupunguza  ushuru, matumaini kwa raia ili kazi hizo  ziweze kudumu na kadhalika.

Viongozi wa Muungano Maarifa tukitaja moja kwa moja kiongozi tendaji John KAVYAVU, kiongozi husika na shauri la uongozi MUHINDO BONANE Abakuk, pamoja naye John TSONGO mwandishi habari walijibu moja kwa moja kwa maswala. Wakihakikishia raia kwamba kazi ni nzuri na itandelea mjini Goma, jimboni Kivu ya kaskazini, nchini DRC na hâta ulimwenguni kote. Na ndilo lengo mhimu la Muungano usio wa kiserkali Maarifa.

Juvénal Murhula.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire