Nyiragongo: Wevi wenyi kumiliki silaha washambulia eneo kadhaa

Exif_JPEG_420

Wevi wenyi kumiliki silaha walishambulia munamo usiku wa tarehe 9 kuamkia tarehe 10 mei mwaka tunao nyumba nne maeneo ya Hewa bora na Kashongo, kijiji Kiziba ya pili, usultani wa Mudja.

Katibu wa shirika la raia tawi ndogo la Kiziba ya pili Bwana Nuru Mwendapole Patient  anena kwamba wevi hao walio miliki silaha,  walijeruhi akina mama moja miongoni mwa watu walioshambuliwa. Pamoja na hayo walipeleka vifaa vingi yaani redio, televisheni, mavazi na kadhalika, wakinyatuka hapo hapo.

Shirika la raia kupitia bwana Nuru Mwendapole Patient lanena kwamba,  ijapo vijana wapiga doria kila leo eneo hilo, usalama mdogo unaendelea kuzorota. Hâta askari polisi hawakuonekana eneo hilo, likiomba viongozi kujihusisha na usalama mdogo pa Kiziba ya pili.

Tukibaki katika ukrasa huu, tueleze kwamba askari jeshi walinasa wanaozaniwa wevi tatu ambao walitaka kuiba ndani ya nyumba usultani wa Munigi, kijiji Ngangi3 eneo  Biirwa usiku wa alhamisi kuamkia ijumaa tarehe 10 mei 2024.

Duru za kijeshi zaeleza kwamba miongoni mwa wevi mwapatikana moja kwa jina la Mussa Fataki Alias kwa maarufu Kabila. Huyu alikuwa akisakwa na askari polisi, kwa kuwa amesababisha usalama mdogo siku nyingi duru za mahali zaeleza.

Duru tu hizo za kijeshi zanena kwamba Bwana Kabila alishutumiwa kujihusisha na mauaji ya kinyozi moja kwa jina la Sekibombo mkaaji kwenyi kijiji Ngangi3. Mwizi huyo alinaswa majira ya saa nne za usiku wakiwa watatu. Moja miongoni mwao ni mwenyi umri wa miaka chini ya kumi na munane.

Juvénal Murhula.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire