Kivu ya kaskazini: Papy Machozi amechaguliwa bila shaka mwana seneti.

Papy Machozi ni kwa sasa moja wa wanaseneti shujaa miongoni mwa wanne, wanaokwenda kuwakilisha jimbo la Kivu ya kaskazini kwenyi chumba cha wana seneti mjini Kinshasa. Akichaguliwa kwa sauti tisa na wanabunge walio wengi jimboni Kivu ya kaskazini hîi juma pili tarehe 26 mei 2024 baada ya mchana kati mjini Goma.  Na hiyo ilimpekea kuchukua nafasi ya kwanza.

Baada ya hapo hali ya shamra shamra ilijitokeza kwa wafwasi, wanamemba wa chama, jamaa, ndugu na marafiki. Mlolongo wa gari ulianza tangu kwenyi chumba cha Bunge kupitia mashanganjia za mji wa Goma hadi kwenyi hoteli Jerrysson.

Huko wakitumia kikombe cha maji kwa furaha wakisherekea ushindi wake mwana seneti Papy Machozi.

Juvénal MURHULA.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire