Akihojiwa na mwana ripota wa gazeti la ronde info, prezidenti wa Muungano wa kamati za soko mjini Bukavu, Etienne BUHENDWA aomba viongozi wa serkali kutumika mkono mkononi na kamati hizo ili kuboresha kazi. Akinena kwamba kamati zilizochaguliwa kwenyi soko kadhaa mjini zaendelea kuchapa kazi bila shaka.
<<Ndio kulikuwa mabadiliko kwenyi kamati zimoja za soko ambayo ni ya kawaida. Viongozi waliochaguliwa tayari wana chapa kazi. Kama kuna wengine ambao wataka kutumika ndani ya kamati, watajitokeza, mhula ya hawa wa mbele itakapokwisha. Mabadiliko yaonekana kwenyi soko kadhaa. Kuna viongozi wapya kwenyi soko ya Kadutu, kwenyi soko Muhanzi, kwenyi soko Nyawera na hapa karibuni ni kunako soko Kamagema pa Panzi. Shirika la raia pamoja na Muungano wa kamati za soko wakiandaa uchaguzi,>>anena prezidenti wa Muungano wa kamati za soko Étienne Buhendwa.
Kuhusu shida zinazokumba wachuuzi, huyu anena kwamba shida ni chungu tele, akitaja mfano wa soko ya Kadutu ambako wacuuzi walipinga kuingia ndani ya soko. Wakipinga labda kupandishwa kwa ushuru na serkali. Labda serkali hakukaa pamoja na wahusika ili wapange pamoja. Ijapo viongozi wa serkali, watetezi wa wacuuzi pamoja idara husika na mazingira wangipata suluhu kwa swala katika amani.
<<Shida ingine ni leadership kati ya viongozi wa serkali na watetezi wa wachuuzi ndani ya soko. Nafikiri kila wamoja wakijua kupanga kazi yao, itakuwa vizuri. Ni kwamba watu wanaingia ndani ya kazi zisizo zao. Kiongozi huenda wa serkali kujiingiza ndani ya kazi ya watetezi na hawa nao labda kujiingiza ndani ya kazi ya kiongozi wa serkali. Hiyo ni shida kubwa. Sisi ni moja wapo wa viungo vya shirika la raia. Tunatumika tukiheshimu kanuni za kazi,>>aeleza Etienne Buhendwa ambaye pia ni prezidenti wa soko la Nguba.
Akiomba mara tena wacuuzi kuungana mkono kwa mkono, ili adui asipate mulango ya kuwasambaza. Kwani ana nguvu kuliko wao. Ni katika lengo la kupigania haki yao.
Etienne Buhendwa asisitiza , akiomba serkali kushirikisha kamati za wachuuzi ndani ya vikao, ili kuzungumza pamoja, na kupeleka habari kwa wahusika mapema, katika kutafuta suluhu kwa hatua zinayochukuliwa.
Juvénal Murhula.
Poster un Commentaire
Vous devez vous connecter pour publier un commentaire.