Ituri: Vijiji kumi vimerudishwa mikononi mwa jeshi la taifa FARDC kwa  mwaka

Jeshi la taifa FARDC limehakikisha kuvirudisha mikononi mwake vijiji kumi wilayani Djugu na Irumu munamo mwaka moja, likisaidiwa na Monusco.

Hayo yalifahamishwa hîi juma tatu mjini Bunia, wakati wa mazungumzo kati liwali mwanajeshi Johnny Luboya N’kashama na mwakilishi  maalam makamu wa Katibu mkuu  wa Umoja wa kimataifa husika na ukingo pia operesheni Vivian Van Perre.

Viongozi hawo wawili walikubaliana kwamba nguvu za pamoja kuhusu operesheni Monusco FARDC zilipunguza machafuko ya kundi zenyi kumiliki silaha jimboni humo. Pia mazungumzo kati ya makabila kwa msaada wa Monusco ilipelekea kusahini makubaliano ya kusitisha vita kwa lote na lundi zenyi kushikilia silaha.

Vivian  Van de Perre aweka mkazo kwa uhusiano kati ya viongozi wa DRC na Umoja wa kimataifa, ajili ya kupunguza ujeuri unaosababishwa na kundi zenyi kumiliki silaha.

Mnenaji wa jeshi jimboni Luteni Jules Ngongo anena kwamba kuzibiti vijiji vingi, kulipelekea wahami wengi kurejea makwao.<< Hakuna tena mashambulizi nafasi waishio wahami, kwa kuwa habari inatembea huku na kule. Hiyo ni kazi kubwa ya Monusco. Tuliendesha operesheni za pamoja ambazo zilitowa matokeo mazuri, >> anena afisa huyu mwanajeshi.

Wakati huo, mwakilishi maalam makamu wa Katibu mkuu wa Umoja wa kimataifa anapanga kukutana na kundi kadhaa za raia, yaani viongozi wa akina mama na wanamemba wa shirika la raia.

Chumba cha wandishi.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire