Siku mbili mfululizo hîi juma nne tarehe 6 agosti, tangu kuanzishwa kwa semina ya mafunzo kuhusu haki ya binaadam. Prezidenti wa shirika la kutetea haki ya binaadam jimboni Kivu ya kaskazini ASVOCO, Dufina Tabu akigusia vipengele kadhaa kuhusu sheria ulimwenguni ya haki ya binaadam. Vipengele hivi vikionekana kukiukwa mara kwa mara na viongozi wa serkali na hâta raia kwa jumla.
Katika kikao hicho na wandishi habari, Prezidenti wa shirika ASVOCO Dufina Tabu anena kwamba wandishi habari wameanza kutambua wenyewe kuwa matatizo ni chungu tele ndani ya sekta ya utetezi wa haki za binaadam.
Akihojiwa kuhusu kufanana kuegemea upande wa Rwanda ambayo yavamia DRC, ijapo DRC haivamie Rwanda, Dufina Tabu anena kwamba yéyé haegemee upande wa Rwanda. << Kwa kweli, watu wenyi wanasoma haki ya binaadam watazani kwamba tunasemea nchi ya Rwanda. Lakini sisi tunatamka kuhusu inayoandikwa ndani sheria ulimwenguni kuhusu haki ya binaadam. Mfano wa kipengele cha 15 kuhusu haki ya binaadam, inayosema: kila mtu anahaki ya kupewa uraia, hakuna anayeweza kumnyanganya mwengine uraia. Si mimi Dufina nasema hiyo ila ni sheria ulimwenguni kuhusu haki ya binaadam. Ukizani kwamba ni wale wenyi kuomba uraia ndio twasemeye, apana. Inabidi tu tuheshimu haki ya binaadam>>, aeleza Prezidenti wa shirika ASVOCO Dufina Tabu.
Akikumbusha kwamba tangu mwanzo wa vita, aliomba watu wakae kwenyi kiti moja, wazungumze ili kutekeleza amani kamili, wakiacha mauaji, ambayo ni jambo lisilofurahisha.
Dufina Tabu aonyesha kwamba sheria ulimwenguni kuhusu haki ya binaadam ilionekana, baada ya vita ya mwaka 1940- 1945. Walitambua kutoheshimu vipengele ndani ya sheria hiyo. Akisisitiza kuheshimu haki ya binaadam na kwamba tutafikia Amani.
Tufahamishe kwamba Bwana Dufina Tabu anaandaa kampeni kuhusu haki ya binaadam nchini Rwanda, ambayo itajumwisha wandishi habari wa kanda la maziwa makuu, yaani Rwanda, Burundi na Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo. Ikiwa muda wa kuondowa mawazo mabovu kuhusu haki ya binaadam ndani ya vichwa vya watu.
Juvénal Murhula.
Poster un Commentaire
Vous devez vous connecter pour publier un commentaire.