Muungano Rasta Ouran umefungua rasmi hîi juma nne tarehe 6 agosti ofisi yake mjini Goma, jimboni Kivu ya kaskazini. Sherehe ilifanyika katika hali ya shamra shamra kwenyi jumba la vijana mjini Goma.
Prezidenti wa Muungano Rasta Ouran Katembo Chaniko wa Thathakulu anena kwamba alikuja mjini, ili kuanzisha rasmi kazi za Muungano Rasta Ouran ambao yéyé ni kiongozi.
<<Mimi nilifika ili kuanzisha rasmi kazi za Muungano Rasta Ouran. Katika lengo la kutaka mtu mweusi afahamu rangi yake . Manake aweze kufahamu utamaduni yake. Na utajiri yaliyomo>>, aeleza Prezidenti wa Muungano Rasta Ouran Katembo Chaniko wa Thathakulu.
Akihojiwa kuhusu tafauti kati ya Rasta Ouran na ma Rasta wengine, prezidenti anena kwamba tofauti inapatikana kupitia lengo. Ma Rasta wengine wakifwata lengo zao, ila Rata Ouran inalengo ya kutafuta mtu mweusi aweze kufahamu rangi yake, afahamu Afrika yake, afahamu mali ama utajiri anayo.
Kwa nini Rasta Ouran atumia lugha za kigeni akijiweka mbali na utamaduni , prezidenti wa Rasta Ouran Katembo Chaniko aeleza kuwa lugha hizo ndizo watu wamefunzwa na ambazo wazisikia vyepesi. Ndio maana inabidi kuzitumia ili kuelewesha watu ujumbe ulioko. Pasipo kutupilia utamaduni wetu.
Rasta Ouran hapige makanisa vita, ila anapinga yule yeyote anayesema kwamba utamaduni wetu ni ulozi. Kwamba kukumbuka tabia za ma babu ni alama ya uchawi.
Kuhusu vita inayokumba DRC, mchango wa Rasta Ouran ni gani, prezidenti aomba watu kuungana bega kwa bega, ili kupiganisha adui, wasitegemee wageni kutoka nje. Kwa kuwa wageni wanapigana kuhusu faida yao wenyewe.
Juvénal Murhula.
Poster un Commentaire
Vous devez vous connecter pour publier un commentaire.