Goma: Hali yaonekana kuwa ya heka heka kutokana na ajali ya barabarani

Hali ni ya heka heka mjini Goma hîi ijumaa tarehe 8 agosti 2024 majira ya saa kenda jioni. Milio ya risasi ilisikika muda wa dakika zaidi ya thelasini,  kwenyi mashanganjia kadhaa mjini humo.

Habari toka hapa na pâle zaeleza kwamba, hiyo ilitokana na gari ya askari jeshi iliyogonga watu pande za mashanganjia Signers. Bila kutowa idadi kamili ya watu waliojeruhiwa ama kufariki dunia. Miongoni mwa wahanga mwapatikana  mwendesha piki piki.

Ndipo wenzake  kukumbwa na hasira, wakiweka vizuizi barabarani. Na hapo hapo,  vyombo vya usalama kufyatuwa risasi, kwa kusambaza waandamanaji.

Hali ya vurugu ilionekana muda wa dakika zaidi hamsini,  watu wakitafuta njia huku na kule, wakikimbia milio ya risasi.

Wafanya biashara wengi kando ya barabara walionekana kunyatuka, wamoja wakipoteza vitu vyao. Wengine waliona ni vema kufunga kazi, wakihofia kupoteza maisha na hâta mali yao.

Ijapo hali kuanza kurudi tulivu mjini Goma, milio ya risasi inaendelea kusikika kwenyi nafasi mbali mbali mjini humo, tukiwa majira ya saa kumi na nusu. Idadi ya watu waliojeruhiwa na hâta kufariki haijajulikana bado.

Juvénal Murhula.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire