Kivu ya kaskazini : Shirika FONECO lapinga kufungua shule ingawa serkali haheshimu haki ya walimu

Habari kutoka shirika la kutetea haki ya walimu FONECO zaeleza kwamba walimu memba wake, hawatafungula shule mwanzo wa mwaka. Kutokana na gisi serkali hajihusishe kwa kuboresha maisha yao, ijapo juhudi zenyi kufanyika ndani ya sekta hiyo  ya maadibisho.

Prezidenti wa shirika FoNECO jimboni Kivu ya kaskazini Fidèle Byuma  anena kwamba walimu wanaendelea kuachiliwa na serkali. Akiomba walimu wa shirika zingine kuungana mkono mkononi, ili kulazimisha serkali kuwapa haki yao. Na kwamba ni vema watu  kujiunga pamoja wakidai haki.

<< Tunatomba serkali kutayarisha vema kufunguliwa kwa shule.  Akiheshimu ahadi kwa walimu. Wenzangu wapenzi, ni muda sasa kwetu kisikilika. Ingawa serkali halipe dola 500 za marekani kwa mwezi, na kwa Mwalimu, inabidi kutofungua shule>>, anena Fidèle Byuma prezidenti wa shirika la kutetea haki ya walimu Kivu ya kaskazini.

Tukumbushe kwamba Raisi wa DRC aliweza kutangaza kusoma kwa bure kwenyi shule la msinji,  alipoingia madarakani, Ijapo hakuweza kutafuta pia mbinu kwa kuboresha mishahara ya walimu, kwa faida ya jamaa zao, ili wafanye kazi bora.

Wandishi habari.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire