Kivu ya kaskazini: Wandishi habari waahidi mchango katika harakati za kutekeleza Amani na usalama

Wandishi habari toka gazeti kadhaa na watumiaji wa mitandao jimboni Kivu ya kaskazini wamecukua hatua ya kuleta mcango wao, katika ujenzi wa nchi, kupitia Vyombo vya habari. Wakikubali kutumika ili kufaulu kwa harakati za kisiasa, amani na usalama nchini DRC.

Walikusudia hayo baada ya kikao kilichoandaliwa na Monusco tawi la kisiasa mjini Goma, Ilikuwa alhamusi tarehe 15 agosti 2024. Baada ya Monusco kushiriki kwenyi harakati za kisiasa ili kutafuta amani  mjini Nairobi na Luanda.

Wakati huo wandishi habari walibadili fikra kuhusu mambo kadhaa; mcango wa vyombo vya habari katika harakati za kisiasa amani na usalama jimboni Kivu ya kaskazini, kutangaza habari za uongo; matokeo na jukumu la mwandishi habari kijamii.

Hawa waligusia pia kazi zilizofanyika na shirika lihusikalo na kupokonya silaha, kuondowa na kuingizia ndani ya maisha ya kawaida wanamugambo waliotumia silaha kinyume na sheria. Pamoja na hayo shida zinazo kumba Monusco katika kazi hizo. Shirika husika na kupokonya silaha ni DDRS, na lile husika na mpango ni PDDRC-S.

Baada ya mchana kati mazungumzo yalihusu harakati za kisiasa nchini DRC, Nairobi na Luanda, halioko kwa sasa kuhusu harakati hizo.

Mwishowe wandishi habari walichukuwa azimio kadhaa, wakiahidi kupitia kazi wanazozifanya kila leo, kwamba wataweza kusindikiza harakati za kisiasa, amani na usalama jimboni Kivu ya kaskazini.

Hawa waliomba Monusco kufanya yote iwezekanayo ili wapate habari za kweli, wakati unaofaa ili kuzitangaza, katika lengo la ujenzi wa taifa.

Tufahamishe kwamba kazi ziliongozwa na wandishi habarî  wa mahali yaani, Tuver Wundi wa RTNC na Papy Okito mwenyeji wa Gazeti Échos d’opinion kwa msaada wa Monusco.

Juvénal Murhula.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire