Kivu ya kaskazini: Wandishi habari wapokea vyeti vyao toka Shirika ASSVOCO

Exif_JPEG_420

Wandishi habari kumi na nne jimboni Kivu ya kaskazini wamepewa vyeti vyao toka shirika la kutetea haki ya binaadam ASVOCO, likiongozwa naye Dufina Tabu Mwenebatende. Hawa walifunzwa muda wa siku tatu kuhusu vipengele kadhaa vya sheria ulimwenguni kuhusu haki ya binaadam.

Viongozi wa serkali hawakushiriki kwenyi sherehe ijapo walialikwa anena prezidenti wa ASSVOCO Dufina Tabu Mwenebatende.

Mimi sina hofu hâta kama viongozi hawakushiriki. Nilijuwa kwamba hawatafika maana hîi ni tabia yao tunapowaalika. Hasa tunapozungumzia mambo kuhusu haki ya binaadam, hawa wafichama anena Dufina Tabu Mwenebatende.

Baada ya hapo, washiriki mafunzo walichangia kikombe cha maji, ili kukamilisha kazi walioifanya muda wa siku tatu.

Kuhusu vita vya M23 na vinginezo Kivu ya kaskazini, prezidenti wa shirika ASSVOCO anena kwamba yéyé haunge mkono vita, inabidi watu kukaa kwenyi meza ili kutafuta suluhu kwa mizozo inayowakumba.

Akiomba serkali pia kuheshimu haki ya binaadam, akiboresha maisha yao ya kila leo, kwa kuwa viongozi hawa wanaendelea kukiuka haki ya binaadam.

Juvénal Murhula.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire